@storika_tv: Uwanja wa Old Trafford ulilipuka kwa mshindo mkubwa wa shangwe! Ilikuwa ni Novemba ya mwaka 2002, na mshambuliaji wa Manchester United, Diego Forlán, alikuwa ametoka kuifungia timu yake goli la ushindi dhidi ya Southampton dakika za jioni kabisa. Akizidiwa na hisia na furaha iliyopitiliza, Forlán alivua jezi yake na kuizungusha hewani kwa fujo. Lakini kabla hata hajafanikiwa kuivaa tena, filimbi ililia na mchezo ukaendelea! Hapo ndipo taharuki ilipoanza Forlán akijikuta anakimbia uwanjani akipiga pasi na kukaba akiwa kifua wazi, huku jezi yake ikiwa mkononi kama kitambaa cha doria. Jambo hili hilitafsiriwa kama utovu wa Nidhamu na kusababisha FIFA kuja na sheria ya kupewa kadi ya njano baada ya kuvua jezi uwanjani #storikatv #diego