@veriafya: Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Nathanael Mtinangi anashauri Wanawake wenye Changamoto ya kupata ujauzito (Wagumba) wasijisafishe moja kwa moja baada ya kushiriki tendo la ndoa ili kutoa nafasi nzuri kwa Mbegu za kiume kufikia yai kwa namba kubwa. Katika mahojiano haya yaliyofanyika kupitia Mwananchi Digital, Dkt. Mtinangi anabainisha kuwa njia hii inaweza kuongeza uwezekano kwa Wanawake hawa kupata Ujauzito