@abt__media: #HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limefanikiwa kukamata malori mawili ya mizigo yakiwa yamebeba shehena ya maboksi 1,962 ya vipodozi vya magendo, vikiwemo vile vilivyopigwa marufuku nchini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, SACP Augustine Senga, amebainisha kuwa magari hayo yamekamatwa kwa nyakati tofauti kupitia misako na oparesheni mbalimbali zilizofanyika wilayani Ileje na katika kituo cha kupimia uzito cha Mpemba wilayani Momba. Katika tukio la kwanza mnamo Mei 27, 2026, polisi walilikamata gari aina ya Fuso (T 605 DJF) wilayani Ileje likiwa na maboksi 1,892 ya vipodozi hivyo baada ya kuvuka mpaka wa Tunduma. Katika hatua nyingine mnamo Juni 4, 2026 asubuhi, polisi walilikamata gari la pili aina ya Howo (T 934 ECY) katika mizani ya Mpemba likitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) likiwa limebeba madini ya shaba, huku likiwa limeficha maboksi 70 ya vipodozi hivyo vya magendo. Jumla ya watuhumiwa wanane wamekamatwa kufuatia matukio hayo, ambapo watuhumiwa wanne walionaswa wilayani Ileje tayari wamefikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria. Kamanda Senga ametoa wito mkali kwa wananchi na wafanyabiashara kufuata taratibu zote za kiforodha zilizowekwa ili kuepuka usumbufu na kadhia za kisheria zinazoweza kujitokeza kutokana na ukwepaji kodi na uingizaji wa bidhaa haramu.#HABARI #abtmedia #abtfilm #HUDUMA_ZAKIFLME_BEI_ZA_KIZAWA

ABT MEDIA
ABT MEDIA
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 05 June 2026 07:49:37 GMT
28931
799
20
42

Music

Download

Comments

ally.mdemu5
Ally Mdemu :
duuh wameisha
2026-06-06 11:30:03
0
amina.abubakary31
Amina Abubakary :
eee mungu nakuita mungu
2026-06-06 03:57:17
0
tinner.maffa
Tinner Maffa :
mhhhh
2026-06-05 20:49:07
1
fredmagunda
Fred Magunda :
mme kazana kukoment tamaa tamaa ...tatizo hamjui utafutaji hiyo ni ajar kazini ...poleni Sana wapambanaji changamoto ni moja ya utafutaji
2026-06-06 04:59:03
8
dogo.brand87
mwampulo :
mwamtege
2026-06-06 12:55:30
0
kiredio94.kitungamtoto
Kitunga Mtoto :
Mmmh tamaa mbaya sana
2026-06-05 18:23:55
1
jordan.kandonga
Jordan Kandonga :
kutafuta watekaji amna ila maisha yawatu ndo mnajua
2026-06-06 02:55:55
1
dantown30
user7782346947487 :
Dola sh 5000 au siyo?
2026-06-06 14:53:17
0
user5183448565834
user casal :
Kaka poleni sana mtatoboatu hakunajambo lisilonamwisho
2026-06-06 17:49:31
0
ayubu.b..maumba
Ayubu B. Maumba :
Kutafuta watekaji aaaah
2026-06-06 04:12:52
0
p.wamchongo
Peter Julius :
sasa mwenye Gari anashida gani
2026-06-06 06:59:41
0
mwaipopo075
mwaipopo :
jamani tamaa mbaya
2026-06-05 20:22:50
0
www.malume4
Toure boy :
jaman madeleva tuache tamaa
2026-06-05 19:01:12
0
user8732721444018
Chinno :
Jamani mimi binafsi nishauri tuu kweli hela tunazitaka sana ila asaivi mizigo ya ambayo sio rasmi haifai kubeba maana Road kwamoto sana
2026-06-06 18:02:23
0
mwadad2
mwadada :
😅😅😅
2026-06-05 18:08:22
0
To see more videos from user @abt__media, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About