@sirizaasili: MAMA PENGWINI HAKUNA KUPOA 🐧 Upendo wa mama hauna mipaka, hata katika ulimwengu wa wanyama. Pengwini wa Tawaki hutumia nguvu kubwa kumlea mtoto wake. Kila siku mama husafiri baharini kutafuta chakula, kisha hupanda mawe, mizizi na njia ngumu za msituni ili kumfikishia mtoto wake chakula. Katika kipindi cha malezi, anaweza kuogelea zaidi ya kilomita 1,000, kutembea umbali sawa na marathoni, na kupoteza hadi nusu ya uzito wa mwili wake. Lakini juhudi zote hizo zina lengo moja tu: kuhakikisha mtoto wake anakua na kuwa tayari kuanza maisha yake mwenyewe baharini. 🎥 Credit: BBC Earth #SirizaAsili #Penguin #Nature #Wildlife #NatureDocumentary