@uniforce_energies: Ukishakamilisha installation, usiache mfumo bila hatua ya mwisho ya uthibitisho. Kuna kitu muhimu sana kwenye projects kubwa za umeme. Third party verification na certification. Baada ya kumaliza kazi, mlete mtu mwingine mwenye uwezo wa kitaalamu afanye: - testing ya mfumo - inspection ya installation - verification ya protection systems - na kutoa certificate ya uthibitisho Hii si formalities tu. Hii ni sehemu ya kulinda kazi yako na mteja pia. Kwa sababu mara nyingi, matatizo yakitokea baadaye, maswali huanza: - Nani alifanya installation - Je fundi alikuwa na sifa sahihi - Je kazi ilikaguliwa na nani - Je standards zilifuatwa Kwenye mazingira ya commercial buildings na systems kubwa, law na responsibility huwa wazi sana. Bila documentation na certification, lawama zinaweza kurudi kwa fundi hata kama alifanya kazi kwa uangalifu. Ndiyo maana kwenye professional practice: - testing si hiari - certification si mapambo - compliance si chaguo Ni sehemu ya kazi yenyewe. Kama una sifa na unafanya kazi kwenye electrical systems, hakikisha pia unafuata taratibu za usajili na leseni zinazotakiwa kufanya kazi kitaalamu. Kazi nzuri pekee haitoshi. Kazi nzuri iliyo documented na certified ndiyo inalinda pande zote mbili. Tufollow kwa maudhui ya kila siku kuhusu: - Electrical Engineering - Installation standards - Safety na compliance - Industrial systems - Professional growth kwenye ufundi