@anibal.alzamora.c3:

Anibal Alzamora Coronado
Anibal Alzamora Coronado
Open In TikTok:
Region: ES
Saturday 06 June 2026 10:57:05 GMT
844
16
0
0

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @anibal.alzamora.c3, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema ndani ya muda mfupi ujao Zanzibar itakuwa inajitegemea kwa nishati ya umeme, hatua itakayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Juma Malik Akil wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya kimkakati ya maendeleo katika sekta ya nishati ya jua na upepo Mkoa wa Kusini Unguja. Amesema Serikali inaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na sekta binafsi katika uwekezaji wa nishati mbadala, hususan nishati ya jua, kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika na kupunguza utegemezi. Aidha, amesisitiza kuwa nishati ya umeme ni chachu muhimu ya maendeleo mengine ya kiuchumi na kijamii Zanzibar, akibainisha kuwa uzalishaji wa megawati 400 hadi 500 utaimarisha mazingira ya uwekezaji na kuondoa changamoto ya upatikanaji wa umeme kwa wawekezaji. Dkt. Akil ameongeza kuwa ndani ya miezi sita kuanzia mwezi Aprili, Zanzibar itaanza kutumia umeme wa upepo, hatua ambayo pia itafungua fursa ya kuuza umeme na kuchangia katika gridi ya taifa ya Tanzania Bara. Akizungumzia ziara hiyo, amesema ni sehemu ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika mwaka wa fedha 2025/2026, ikiwa ni maandalizi ya bajeti mpya ya mwaka 2026/2027. Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Nadir Abdul-latif Alwardi, amesema Serikali chini ya uongozi wa Hussein Ali Mwinyi imeendelea kutoa fedha kuhakikisha miradi ya umeme inatekelezwa kwa ufanisi ili wananchi wapate huduma hiyo kwa uhakika na bila ya usumbufu. #zanzibar🇹🇿 #HabariZaZanzibar #zanzibartiktokers #AsamMedia #Zanzibar #fyp #ASAMOnlineTV

About