@okulyjulius: *AHADI IMETIMIA, TABASAMU LIMEREJEA* WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba leo, Juni 7, 2026 amemkabidhi kiti mwendo kipya Bi. Elizabeth Mnyeke, mkazi wa Mkoa wa Iringa, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa baada ya kupokea ombi lake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Isimani mkoani Iringa uliofanyika Juni 5, 2026. Kukabidhiwa kwa kiti hicho kutamwezesha Bi. Mnyeke kutekeleza shughuli zake za kila siku kwa urahisi zaidi na ni sehemu ya dhamira ya Serikali ya kuwagusa na kuwasaidia wananchi wenye mahitaji mbalimbali katika jamii.