@mwl.emilian.katub7: Mungu anasema na wewe tena kupitia madhabahu hii kwamba yale yaliyokufa kwenye maisha yako anayainua na kuyafufua tena Habakuki 3:2 Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema. Leo mwambie Mungu maneno haya Bwana fufua kazi yako katikati ya miaka kwenye maisha yangu, chochote ulichokianzisha ndani yangu na kwenye maisha yangu ambacho kimekufa, Bwana naomba ukifufue tena katika jina la Yesu Nimekuombea Mungu wa Israeli afufue kazi yake kwenye maisha yako kabla mwaka huu haujaisha, chochote kilichokufa kikainuke tena katika jina la Yesu