@afyawarrren: Tatizo la masikio kupiga kelele kitaalamu hujulikana kama Tinnitus. Hali hii humfanya mtu kusikia sauti zisizo kutoka nje, kama vile mlio, filimbi, au mngurumo ndani ya sikio. 🔎 Dalili zake ✍Kusikia mlio wa kelele au filimbi masikioni ✍Sauti inaweza kuwa ya kudumu au ya muda ✍Wakati mwingine huongezeka ukiwa kimya ⚠️ Sababu za masikio kupiga kelele ✍Maambukizi ndani ya sikio – bakteria au fangasi huathiri usikivu ✍Ajali au majeraha – hasa kwenye kichwa au sikio ✍Sikio kujaa maji – huweza kuziba njia ya sikio ✍Kusikiliza muziki kwa sauti kubwa – huharibu mishipa ya sikio ✍Nywele ndani ya sikio kupinda – huchangia kuziba au kuwasha 🚨 Mambo ya kufanya ✍Epuka kelele kubwa na tumia earphones kwa tahadhari ✍Hakikisha sikio linabaki safi na kavu ✍Pata uchunguzi wa kitaalamu mapema