@millardayo_: Waziri wa Fedha, Balozi Khamisi Mussa Omar amesema Serikali inapendekeza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 5 kwenye thamani ya dau la kamari (gaming) linalochezwa kupitia michezo ya kubashiri ya ardhini au mtandaoni, michezo ya kasino ya ardhini au mtandaoni, mashine za sloti pamoja na michezo ya vikaragosi (virtual games operations). Akiwasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Waziri Khamisi amesema hatua hiyo inalenga kupunguza madhara yanayotokana na michezo ya kubahatisha, ikiwemo uraibu wa kamari na kupungua kwa nguvu kazi ya Taifa kutokana na baadhi ya Vijana kujihusisha zaidi na michezo hiyo badala ya shughuli za uzalishaji na maendeleo ya kiuchumi. Amesema pia kuwa asilimia 10 ya mapato yatakayokusanywa kutokana na ushuru huo wa asilimia 5 yatawasilishwa kwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) ili kuongeza ufanisi katika usimamizi na udhibiti wa sekta ya michezo ya kubahatisha Nchini. Kwa mujibu wa Waziri huyo, hatua hiyo pamoja na kusaidia kudhibiti athari za kijamii zinazotokana na kamari, pia itaongeza mapato ya Serikali yatakayosaidia kugharamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo na uchumi. Amesema pendekezo hilo linatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 74.50.

millardayo
millardayo
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 11 June 2026 14:44:19 GMT
2829
144
3
4

Music

Download

Comments

sciper26
Sciper💙🌀 :
This is not looking good😒😅
2026-06-11 14:55:36
0
missmars14th
Márs🌹🪐 :
😂😂🤣Wawekezaji Hoyee✊✊
2026-06-11 14:49:00
0
meshackkabuje
meshack kabuje :
wanangu wa kubet apa 😂😂
2026-06-11 14:51:37
0
To see more videos from user @millardayo_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About