@officialruby_: Watu wengi hujilaumu kila wanaporudia tabia ambayo walikuwa wameamua kuacha. Husema: ❌ “Sina nidhamu.” ❌ “Mimi ni dhaifu.” ❌ “Nimeshindwa tena.” Lakini ukweli unaweza kuwa tofauti. Tatizo mara nyingi si ukosefu wa nidhamu. Tatizo ni kwamba mazingira yanayokuzunguka bado yanachochea tabia ile ile kila siku. ⚠️ Simu ipo kitandani kila usiku. ⚠️ Stress bado ipo. ⚠️ Upweke bado upo. ⚠️ Vishawishi/ Triggers bado zipo. ⚠️ Muda wa ziada hauna matumizi. Na kila kishawishi/ trigger inapojitokeza... ubongo unarudi kwenye tabia uliyoizoea. Kumbuka: Mabadiliko ya kweli hayaanzi kwa motivation. Yanaanza kwa kubadilisha mazingira yako ya kila siku. Usijenge maisha yanayokulazimisha kupambana na majaribu kila saa. Jenge maisha yanayopunguza majaribu yenyewe. 👇 Kwa maoni yako, ni nini kinachowarudisha watu wengi zaidi? 1️⃣ Stress 2️⃣ Upweke 3️⃣ Simu 4️⃣ Kukosa shughuli Andika jibu lako kwenye comments #recoveryjourney🙌❤😍💪💯 #mentalstrengthtraining #personalgrowth #mindsetshift #focusongrowth