@lokomatv: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameagiza Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigamboni kumkamata kwa kumshikilia Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Lingato, Kata ya Kisarawe II, Cosma Kulwa maarufu kama Kalimanzira, kwa tuhuma za kuuza viwanja mara mbili na kusababisha migogoro ya ardhi kwa wakazi wa eneo hilo. Chalamila alitoa agizo hilo leo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Wilaya ya Kigamboni. Akiwa katika Mtaa wa Kichangani akitatua mgogoro wa ardhi unaohusisha zaidi ya familia 23 na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), mwananchi mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan alijitokeza na kutoa malalamiko dhidi ya mwenyekiti huyo, akimtuhumu kumuuzia eneo la ekari moja ambalo baadaye lilidaiwa kuuzwa kwa mtu mwingine. Kwa mujibu wa madai yaliyotolewa na wananchi, mwenyekiti huyo amekuwa akihusishwa na uuzaji wa viwanja vyenye migogoro pamoja na viwanja ambavyo tayari vilikuwa vimeuzwa kwa wanunuzi wengine, hali inayodaiwa kuchangia kuongezeka kwa migogoro ya ardhi katika eneo hilo. Baada ya kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu nyaraka za mauziano zinazodaiwa kuhusika katika sakata hilo, Chalamila aliamuru akamatwe mara moja na kuwekwa mahabusu. "Akamatwe na akawekwe mahabusu mpaka kesho. Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, kesho itisha mkutano wa hadhara wa wananchi. Huyu mwenyekiti kesho atoke mahabusu akiwa na pingu ahudhurie mkutano huo. Amesema Chalamila #viral #tiktokindia #shots #trending #reels
Lokomatv_
Region: TZ
Thursday 11 June 2026 19:15:25 GMT
Music
Download
Comments
Cheetah boy 🐆小王翻译 :
who is this guy🤣
2026-06-12 06:46:28
2
Said Ally :
asantesana baba yan hayo ndootonayataka
wananchi wako tz
mungu akuongoze 🤲🤲
2026-06-12 11:57:01
2
D :
asante
2026-06-12 10:26:30
0
innocentmbamba2 :
nimeckia Asante kutoka kwa mama
2026-06-12 06:00:11
1
Sulayman Abdulrahman :
Nimeipenda hii
2026-06-12 07:13:12
1
betterhelthvibe :
Mungu tunusuru na matapeli
2026-06-12 06:57:10
0
Nasma Grey :
Mmmh mungu wangu mm kwangu huko mwaka sijaenda kutembelea
2026-06-12 07:15:02
0
Hulleynah James :
R.I.P mpenja 🤣🤣🤣🤣
2026-06-12 07:40:20
1
Issa :
Wenyeviti wasee sana kmmk
2026-06-12 05:36:55
1
Mahava_home_elegance :
Jamn mtendaji Jumbe
2026-06-12 10:21:22
1
Masha steel :
huuu upuuzi upo sana nchi hiii
2026-06-12 06:19:29
2
Gee :
Utapeli live
2026-06-12 09:05:44
1
Phyna de Wille :
saf😂
2026-06-12 05:13:17
1
Salu Masoni :
limeisha hilo
2026-06-12 05:23:26
1
Adam Mkalimbe :
mkuu nakuombea kwamungu akulinde unataka haki
2026-06-12 04:06:02
1
makambimaestro540 :
washa tv mpe soda😂
2026-06-12 07:59:56
0
saddbrand01 :
DAH HII BARABARA SIAMINI
2026-06-12 09:00:16
0
mjuni03 :
Ccm Ccm
2026-06-12 09:09:20
0
𝐏𝐚𝐩𝐢𝐥𝐢𝐭𝐨 :
Ad TV 📺 😂😂😅
2026-06-12 12:27:53
0
 :
ASANTE😂
2026-06-12 07:43:14
0
mrpaul304 :
Charamila Nimekukubari sanaaa
2026-06-12 07:23:16
0
khamiskhamis341 :
🥰🥰🥰
2026-06-12 09:05:27
0
cholo🇲🇻 🇲🇻 🇲🇻 :
🫡 🖖 🫡 🖖 🫡 🖖 🫡 🖖
2026-06-12 12:54:27
0
WISE BIGALLEFTI :
😅😅😅😅😅😅😅😅😅
2026-06-12 02:01:50
0
To see more videos from user @lokomatv, please go to the Tikwm
homepage.