@kingnyorobi1: DHAMBI INAYOITESA TANZANIA HAIONEKANI KWA MACHO, AMBAPO SHETANI HAKUSAMEHEWA KWAYO Na, King Nyorobi ASKOFU Mkuu wa kanisa la Ufunuo Tanzania Dkt Paul Bendera amesema kuwa Dhambi inayolitesa taifa la Tanzania ni Dhambi ambayo haionekani kwa macho na kama ingekuwa inaonekana basi taifa lingedumu na kudumisha Amani Mshikamano na umoja wa Kitaifa” Askofu Bendera aliyasema hayo alipopata nafasi ya Kufanya Maombi Mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia suluhu Hassani kwenye Tukio la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Benk kuu ya Tanzania June 12, 2026 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere (JNICC )Jijini Dar es salaam. Katika Maombi hayo Askofu alisema kuwa “Dhambi inayotesa taifa letu haionekani kwa macho na ingekuwa inaonekana kwa Macho taifa letu lingedumu na kudumisha Amani, Mshikamano na umoja wetu wa Kitaifa” Aidha Askofu Bendera alimwambia Rais Samia “Tatizo letu, wengi Unaowapigania, unaowainua na kuwafanya wawe mbele yako, wengi wao wanakushangaza wanapobadilika, nakuombea Mungu akupe maisha marefu na akupe watu wema watakaotukusanya sisi kama Taifa tuzidi kudumu na kudumisha Amani ya Taifa”. Askofu Bendera alifafanua kwa Kilichomuangusha Shetani sio dhambi ya kuonekana ndio maana hakusamehewa ni dhambi iliyokuwa ndani na kudai kuwa ile Dhambi ni mbaya zaidi lakini ingekuwa ya kawaida kama Adamu na Hawa ingesameheka. “Nawashauri viongozi wote wanaolitumikia Taifa letu wajitahidi kuomba Neema ya Mungu izidi kuwa juu yao” Askofu Bendera aliwasihi Watumishi Mbalimbali wa Umma. MWISHO
kingnyorobi
Region: TZ
Friday 12 June 2026 12:43:22 GMT
Music
Download
Comments
𝔸𝕣𝕠𝕪𝕔𝕖👊 :
Rais wangu mwanamke shupavu🥰
2026-06-13 06:57:31
2
patanishouvumi :
Amina Baba
2026-06-12 18:46:55
1
rey 98 :
Amen daddy 🥰🥰🥰🥰🙏
2026-06-12 13:17:57
2
FUNDI FURNITURE :
Ameen Father
2026-06-13 18:14:10
0
💥Àlly_gøølïyê💥wányàmwézï øg& :
njaa
2026-06-12 13:03:47
1
onesmohaule1 :
Amen 🙏
2026-06-12 19:35:25
0
Mr. jerusalem :
Yuda
2026-06-13 10:36:30
0
lyjane 🥰😍🥰 :
Amen daddy of mine
2026-06-12 20:48:08
0
katureebe julius :
amiina
2026-06-12 19:58:24
0
pretty queen 👸 ✨️ :
🙏🙏🙏
2026-06-13 05:51:07
0
Mama P..little Precious :
@60MilesTz
2026-06-12 18:09:53
0
Diana Meja :
🥰🥰🥰🙏🙏
2026-06-12 20:53:40
0
To see more videos from user @kingnyorobi1, please go to the Tikwm
homepage.