@wepesitv: Huzuni imetawala Jijini Dodoma baada ya wanafunzi wawili wa chuo cha St.John's ambao ni Rebeca Misungwi na Felista Peter Fransis kufariki kwa ajali ya Moto uliotokea katika chumba walichokuwa wanaishi, huku Chanzo cha tukio la Moto huo ukihusishwa na Wivu wa Mapenzi. Inaelezwa kuwa Moto huo uliwashwa na Mpenzi (Boyfriend) wa mmoja ya wanafunzi hao (Felister) Boyfriend ambae pia ni Mwanafunzi wa Chuo kikuu hicho cha St John's. Rebeca Misungwi alifariki dunia tarehe 11 Juni, huku Felister amefariki dunia Juni 13 wakati akiendelea na matibabu katika Hosptali ya Kanda ya Benjamin Mkapa ya Jijini Dodoma. Tukio la Moto huo, lilitokea usiku wa tarehe 6 na Mwili wa Rebeca umesafirishwa Jana kuelekea Wilaya ya Magu Jijini Mwanza kwa maziko. Kwa upande wa jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limethibitisha kutokea kwa tukio la moto ulioteketeza chumba cha wanafunzi wa chuo cha St. John jijini Dodoma, na kusababisha vifo vya wanachuo wawili. Powered by #MGENDISUPERMARKET #THEFINESTCITY 👍 Like | 💬 Comment | 🔁 Share