@jamiivoice_: HABARI: Francis Nyakurwa kutoka Arusha ameiomba Serikali kumsaidia baada ya kuondolewa kazini mwaka 2018 akiwa mwalimu, kufuatia madai kuwa alipandishwa madaraja kimakosa. Akizungumza leo Juni 14, 2026 mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kinampanda, Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Nyakurwa amesema amekuwa akifuatilia suala hilo kwa miaka kadhaa bila kupata suluhisho. Amesema alifanya kazi ya ualimu tangu mwaka 2006 hadi alipoondolewa kazini mwaka 2018 kwa madai kuwa alipandishwa madaraja bila kustahili. “Nilifika sehemu mbalimbali ikiwemo halmashauri, TAMISEMI, Wizara ya Utumishi na taasisi nyingine. Lakini nikaambiwa natakiwa kulipa zaidi ya shilingi milioni 16 ili nirejeshwe kazini kwa madai kuwa nililipwa kinyume cha utaratibu tangu mwaka 2012 nilipoanza kupandishwa madaraja,” amesema Nyakurwa. Akijibu kero hiyo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameonyesha kutoridhishwa na uamuzi huo na kuagiza wahusika waliomuidhinishia kupandishwa madaraja watafutwe na waeleze sababu za kufanya hivyo kama kweli hakustahili. Amesema si sahihi kwa mtumishi kuadhibiwa kwa makosa ya mfumo au ya viongozi waliokuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi hayo. Waziri Mkuu ameongeza kuwa tukio hilo linaashiria uwepo wa uonevu na huenda likahusisha ubadhirifu wa fedha za umma, akisisitiza kuwa Serikali haitakubali vitendo vya aina hiyo kuendelea.

Jamii Voice
Jamii Voice
Open In TikTok:
Region: TZ
Sunday 14 June 2026 15:22:21 GMT
243156
8136
343
333

Music

Download

Comments

chris.charles507
Chris charles :
yaani kama namuona magufuri mwingine ajaye, Salute kwako Mwigulu Nchemba
2026-06-14 18:24:38
93
wilmina11
wilmina :
jaman😭😭😭 Haki za watu zitatendeka kwa kupitia viongozi tuliopewa na Mungu❤️❤️❤️
2026-06-14 16:57:11
50
chole6706
chole :
mungu mlinde sanaa uyu wazirii ilikuaga wap
2026-06-15 06:24:28
32
job.harry
Job Harry :
mzee Mwigulu utafika mbali sana na Mungu atakubalik sana
2026-06-14 17:53:04
34
user9981708796226
Moshi dotto :
Safi sana waziri mkuu🙏
2026-06-14 19:55:18
21
agnesr722635845468
AGNES22635845468 :
daaaaa baba mungu akutunze Yani ww ni makufuli
2026-06-15 05:45:02
14
john.lukumay
John Lukumay :
Safi sana waziri mkuu wetu
2026-06-14 17:10:37
16
rebeccasamuel59
rebby :
eee mungu wa mbinguni msaidie hyu baba🥰🥰🥰🥰 afike mbali
2026-06-15 10:01:25
11
user4267579045121
yule boy :
mungu akulinde mukozi wa watu
2026-06-14 20:06:56
6
samehegerson3
samehe mwinuka :
Asante mkuu upo vzr Mungu akubariki
2026-06-15 08:52:20
6
monicah.mariki
Monicah Mariki :
Asante Waziri Mkuu.Mungu ametuhurumia tumeweza kukupata.
2026-06-15 02:13:08
6
elizabeth.ndimila4
Elizabeth ndimila :
kabisa baba mungu akutie nguru kiatu umekivaa kwer
2026-06-14 17:06:45
6
farhyas.grandma
farhya,s grandma :
kidumu chama tawala ❤️
2026-06-14 18:59:32
5
twiso.natural.herb
Twiso Natural Herbs :
Mwalim. wangu wa bys
2026-06-14 16:47:15
5
user3367530731481
Khadija James faim :
yaani mungu amtunze huyu baba
2026-06-16 07:23:34
3
user19509834469570
user19509834469570 :
waziri mkuu Mungu akutunze
2026-06-16 10:57:41
2
noely.p.h7
noely p h :
au ndo magu wa pili huyu mbona wa moto ivi mungu akulinde na kukupa nguvu na ujasiri uwasaidie wengi mweshimiwa we2💗💗💗💗💗💗💗💗💗
2026-07-02 08:45:00
1
janetwatel1
Watery :
Mungu akuweke miaka mingi babaaa
2026-06-17 17:23:35
1
chammy159
Chammy :
Nakupenda sana Baba Mwigulu
2026-06-14 18:15:47
6
joachim.mathias
Joachim Mathias :
Leo nimekuelewa akili nyingi
2026-06-15 09:01:28
3
benson.mbise
Bensoni Viwanja Arusha :
goooood
2026-06-16 09:39:03
1
linah92051
Linah :
mungu akutunze uishi miaka 10000
2026-06-22 05:37:22
0
debora.mallya
Debora Mallya :
baba mungu akutunze
2026-06-14 18:03:02
1
jemaisaac475
Jema Isaac :
barikiwa baba
2026-06-15 16:30:53
1
annav4662
💐Anna🔒💖💵 :
Asante MUNGU kwa kutuletea Magufuli wa pili 👏
2026-06-19 07:34:12
1
To see more videos from user @jamiivoice_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About