@healthyfity1: Ushawahi kusumbuliwa na maumivu makali ya tonsillitis hadi ukashindwa kula au hata kuongea vizuri? Maumivu ya tonsillitis yanaweza kuwa makali kiasi cha kufanya shughuli za kawaida kuwa ngumu. Watu wengi hupata: Maumivu makali ya koo wakati wa kumeza Ugumu wa kula au kunywa Sauti kubadilika au kuwa nzito Homa na mwili kuchoka Kuvimba kwa tonsils na koo Maumivu yanayosambaa hadi masikioni Harufu mbaya ya mdomo Tatizo huwa kubwa zaidi pale linapojirudia mara kwa mara au linapoachwa bila kushughulikiwa mapema. Je wewe unasumbuliwa na dalili gani sana sana?? #sorethroat #tonsilitis