@sportshqtz: 🌟🇲🇦 UMRI NI NAMBA TU! AYYOUB BOUADDI AWAACHA WENGI MIDOMO WAZI Akiwa na umri wa miaka 18 pekee, Ayyoub Bouaddi ameendelea kuonyesha kwa nini anatajwa kuwa moja ya vipaji vikubwa vinavyochipukia kwenye soka la dunia. 🔥⚽ Dhidi ya Brazil, kijana huyu alionyesha utulivu, kujiamini na ubora wa hali ya juu uliowafanya wengi kuamini kuwa ana maisha marefu sana kwenye soka la kimataifa. 👏 Watangazaji Ghalib Mzinga na Ayoub Hinjo walimchambua kwa kina usiku wa leo, na ni wazi wengi wameondoka na jina lake vichwani mwao. 🌍 Kipaji, maono ya mchezo na ujasiri wa kucheza dhidi ya wakubwa wa dunia akiwa na miaka 18 tu! 💬 Je, umepata nafasi ya kumtazama Ayyoub Bouaddi leo? Unaona anaweza kufika kiwango gani kwenye soka la kimataifa? 👇 #SportsHQ #WorldCup2026 #AyyoubBouaddi #Morocco #Football