@veriafya: Dkt. Nazareth Mbilinyi, Bingwa wa Magonjwa ya Watoto, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya katika Mdahalo wa “Waandae Watoto wako katika Dunia inayobadilika” ulioendeshwa na Hospitali hiyo anabainisha Makuzi ya mtoto si kimo na uzito tu, bali ni pamoja na afya ya akili na ustawi wa kijamii. Takwimu za WHO na UNICEF zinaonesha asilimia 40 ya watoto duniani wanashindwa kufikia uwezo wao kamili kutokana na mazingira mabaya na ukosefu wa ushirikiano kutoka kwa wazazi wao. Ili mtoto akue vizuri, anahitaji mfumo wa "Nurturing Care" unaobeba nguzo tano ambazo ni afya, lishe, ulinzi, kujifunza mapema, na malezi yenye mwitikio chanya. Kujibu maswali ya mtoto kwa upendo na kumwacha acheze ndiko kunakojenga na kuimarisha ubongo wake.