@justine9_joint_care_: Piriformis Syndrome 🦵⚡ Piriformis syndrome ni hali ambapo misuli ya piriformis (misuli iliyopo ndani ya makalio) inakuwa imekaza, imevimba au inaudhi mshipa wa sciatic nerve unaopita karibu nayo. Dalili zinaweza kuwa: ✔ Maumivu ndani ya makalio 🍑 ✔ Maumivu yanayoshuka nyuma ya mguu (kama sciatica) ✔ Ganzi au kuwashwa mguuni ⚡ ✔ Maumivu kuongezeka ukikaa muda mrefu ✔ Maumivu wakati wa kutembea, kupanda ngazi au kukimbia Sababu zinazoweza kuchangia: ✔ Kukaa muda mrefu ✔ Mazoezi makali au kurudia harakati nyingi ✔ Misuli ya makalio kuwa dhaifu au kukaza ✔ Jeraha eneo la makalio Tofauti na Herniated Disc: * Piriformis syndrome: tatizo linaanzia kwenye misuli ya makalio inayoweza kubana neva. * Herniated disc: tatizo linaanzia kwenye diski ya mgongo inayoweza kugusa neva. Msaada unaweza kujumuisha: ✔ Kunyoosha misuli ya piriformis ✔ Mazoezi ya kuimarisha makalio ✔ Kuepuka kukaa muda mrefu ✔ Physiotherapy ikiwa inahitajika. +255672441815 #bac#backpainr#piriformissyndrome