@almecky_tz: Familia ya aliyewahi kuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho imejitokeza kukanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa amefariki Dunia. Kupitia taarifa iliyotolewa na Mwanawe, Ramadhan Pandu Ameir Kificho imeelezwa kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote, kwani Pandu Kificho yupo hai na kwa sasa anaendelea na mapumziko Nyumbani kwake eneo la Mpendae baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi Lumumba. Ramadhan amesema Baba yake alikuwa amelazwa Hospitalini kwa ajili ya Matibabu kufuatia kusumbuliwa na maumivu ya mbavu, ambapo alipatiwa huduma stahiki za kitabibu na baadaye kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya hali yake kuimarika. Aidha, ameonesha masikitiko yake kutokana na kuenezwa kwa taarifa za uongo kuhusu afya ya kiongozi huyo, akisisitiza umuhimu wa wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuthibitisha taarifa kupitia vyanzo rasmi kabla ya kuzisambaza ili kuepuka upotoshaji na taharuki isiyo ya lazima. #Zanzibar #Tanzania #Habari #Football #Trending