@taarifa_24: UTEKAJI WAFIKIA KWA WATOTO WADOGO Watoto watatu wa familia moja, wakazi wa Kijiji cha Kilimahewa wa Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi waliopotea Juni 8, 2026 wakiwa njiani kwenda madrasa wamekutwa wamefariki dunia kwa kunyongwa. Watoto hao ni Kulwa Mohamed (7) na Doto Mohamed (7), wanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Mitopitopi pamoja na Rehema Mohamed (6), mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Mpanyu. Miili ya watoto hao ilipatikana kwa nyakati tofauti ambapo miwili ilipatikana Juni 13, 2026 na mmoja ulipatikana asubuhi ya jana Jumapili Juni 14, 2026 yote katika Pori la Kijiji cha Kilimawe. Jana Jumapili, Juni 14, 2026, miili ya watoto hao ilizikwa ambapo viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi (RC), Zainab Telack walishiriki. Akielezea tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori alisema watoto hao walitoka nyumbani kwao Juni 8 kwenda madrasa ambako taarifa walizonazo hawakufika na kupotelea njiani ambapo walianza msako kuwatafuta.
Taarifa24
Region: ZA
Monday 15 June 2026 11:10:55 GMT
Music
Download
Comments
mamacarotz :
mungu wetu tunaomba msaada wako
2026-06-15 12:00:19
108
kashy :
HASBIALLAHU WANEEMAL WAKIL 😭😭😭
2026-06-15 14:28:07
32
Selina Manase :
ndo mkoa gani jamani poleni sana jamani
2026-06-15 14:38:25
2
neemadavid935 :
Hivi ni nini hiki jamani uwiiiiii 🙌🙌😭😭
2026-06-15 13:14:43
51
gift mwanga :
binaadam tuna roho mbaya sana
2026-06-15 12:37:05
38
Queen_malice💜💜 :
mama yetu Samia Asante kwa ULINZI wako na Usalama.🙏 Hali NI Swali mama
2026-06-15 13:01:48
56
catherahma :
MUNGU WANGU TULINDIE WATOTO WETU TUPO MAKAZIN TUKIWATAFTIA RIZKI😢😢
2026-06-15 13:35:30
34
Balnelly@cakes and bites :
Inamaana ni watoto wa mama moja
2026-06-15 12:54:35
29
precious P💞💕 :
MUNGU nilindie mwanangu na vile shule yao iko polin jmn bila ww MUNGU atuwez
2026-06-15 12:48:40
22
raphaelamsola :
hawa watoto walikosa nn jaman eemungu😭😭🙏🙏
2026-06-15 12:41:24
33
lilianambokile :
mungu mpe nguvu huy mama 😭😭
2026-06-15 12:13:24
18
Leila Fransisy :
mungu tunaomba tetea nchi ya Tanzania😭😭😭😭😭
2026-06-15 12:31:10
21
Ceci👠👔👗🧳💼🌂🧢👓💉🕰️🇹🎒 :
Mungu tulindie watoto wetu🙏
2026-06-15 13:39:08
10
Evaristbenedict99 :
poreni sana wazazi wawatoto hawa😭😭
2026-06-15 14:47:57
5
love :
poleni sana wazazi mungu awatie nguvu
2026-06-15 13:25:08
7
Maryy Benjamini :
pole Sana kwa family😭😭😭
2026-06-15 14:53:02
1
user4887326883545mwahawa mosta :
poleni
2026-06-15 14:58:13
1
q, chilla :
poleni
2026-06-15 14:58:05
0
Leyla Shirima :
Nalia mie jamani tunazalia wauwaji
2026-06-15 12:39:56
9
Naomi Joel :
eeeh Mungu nn kipo duniani😭😭
2026-06-15 12:27:29
6
safinaramadhani45 :
inallilah wainalillah lajiun mungu tujalie mwixho mwema waja wako inshaallah
2026-06-15 13:03:02
7
Graceous Sangah :
mungu tulindie watoto wetu uwiiiii
2026-06-15 13:21:49
7
Da Mamu🥰 :
subhanallah mungu atusaidie kwa watoto wetu hwao wamekosea nn sasa😳😳
2026-06-15 13:52:47
7
Archie :
Jamani 😢 poleni sana 😢
2026-06-15 17:09:32
1
joerysaimoni :
daaaaa
2026-06-15 15:32:47
1
To see more videos from user @taarifa_24, please go to the Tikwm
homepage.