@emagadula01: Ili usiwe mtu wa madeni ni lazima utoke kwenye akili ya madeni uingie kwenye akili huru ambayo itakufanya madeni yaishe Kama umechoka kuwa na madeni chungu nzima fanya hivi 1. Epuka kukopa kwenye kausha damu, hizi zinazoitwa Microfinances. Kukopa kwenye kausha damu ni kosa kubwa ambalo unaweza kulifanya na likagharimu pesa zako nyingi. Microfinances zinatoza ruba kubwa, kuendelea kukopa kule ni kujipalia mkaa, ni bora utafute mbinu mbadala ukope hata kwa marafiki badala ya Microfinances 2. Epuka kukopa kwa njia ya simu kwenye App zinazokopesha na hata hizi Songesha, au Niwezeshe. Hizi pamoja na kukutoza riba kubwa lakoni kuna makato ya simu ambayo huyapigii hesabu ambayo pia yanakugharimu pakubwa bila kujua na yanaendelea kukuweka kwenye madeni ya kudumu siku zote 3. Kama una madeni mengi yanazozalisha riba kila kukicha, Tafuta mkopo mmoja mkubwa wa riba nafuu halafu yalipe hayo madeni madogo madogo yote. Ni bora ukabaki na deni moja kubwa lenye riba nafuu kuliko kuwa na vimadeni vingi vingi ambavyo vinakupa mawazo na vinatoza riba kubwa. 4. Epuka kufanya top up, yaani kuhamisha deni kutoka bank moja kwenda nyingine. Hii nayo ni hatari kubwa sana ambayo naona watumishi wengi wanafanya. 5. Epuka michezo ya bahati au upatu kama vile Betting na Kindege Michezo hii inakuahidi kupata pesa na huku ukiendelea kupoteza fedha zako, kama.uko kwenye madeni ni rahisi sana kujikuta unacheza michezo ya bahati ili ubahatike kumbe ndo unajiingize kwenye dimbwi kubwa la maji ufe. 6. Punguza matumizi yasiyo ya lazima. Matumizi yasiyo ya lazima Kama kukaa online 24/7, kununua vitu visivyo vya lazima nk yanaweza kuendelea kukuweka kwenye hali ya madeni ya kudumu. Usinunue vitu kwa mihemko kilakitu kiwe ndani ya budget 7. Acha kuhonga, kulewa kupita kiasi, na kwenda club. Bila msingi. 8. Achana na roho za ushirikina, uganga na uchawi maana hizo roho na madeni ni hivi 9. Mtangulize Mungu Mbele katika kila hatua, sali asubuhi, mchana na jioni uondokane na roho hiyo ya madeni #fy
Emmanuel Magadula
Region: TZ
Monday 15 June 2026 14:56:57 GMT
Music
Download
Comments
Paulo Mshokela :
ndio
2026-06-16 08:28:30
2
Hamad Magawa :
ubalikiwe sana
2026-06-16 18:56:20
0
Mwanne Magesa :
asante
2026-06-16 05:35:52
4
KIDOMAYO :
amin 🙏🙏🙏
2026-06-16 16:34:47
2
doro_mkomochi :
amina
2026-06-16 20:23:41
1
Magreth Kaguo :
Asante
2026-06-16 03:39:44
2
double d :
amen
2026-06-16 11:21:08
1
Damian Saru :
Amen
2026-06-16 10:55:57
2
Edithagb068587 :
aminaa
2026-06-16 09:46:41
2
user7907421804327 :
asante nimepokea
2026-06-16 10:13:52
2
Wema Wiston :
ameen
2026-06-16 22:40:36
0
user5548828029541 :
ok
2026-06-16 09:29:12
1
William :
ahsante sana ushauri mzuri
2026-06-16 22:35:16
1
LUKE BOY :
Ushauri mzuri
2026-06-16 20:26:24
0
Angelista Nyalusi :
ameni
2026-06-16 12:27:14
0
Tipical 47 :
santehhh
2026-06-16 07:33:29
2
Mama P :
Asante
2026-06-16 09:33:38
2
Elizabeth Mgalula :
asanteee
2026-06-16 16:47:59
1
Kayala mwasi :
🙏🏾🙏🏾
2026-06-16 06:58:17
2
Muhamed Motivation :
👍
2026-06-16 04:43:23
2
Blandina Bugomba :
🔥🔥🙏🙏
2026-06-16 02:02:46
2
LUHANGANO :
🙏🙏🙏
2026-06-15 18:59:08
1
TZ Man :
🔥🔥
2026-06-16 07:09:55
2
To see more videos from user @emagadula01, please go to the Tikwm
homepage.