@jamiivoice_: Bungeni: Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma amewaonya baadhi ya wabunge wa Zanzibar kujiepusha na kauli na mijadala inayoweza kuleta mgawanyiko na kuhatarisha Muungano wa Tanzania. Musukuma ametoa onyo hilo leo bungeni alipokuwa akichangia mjadala kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka wa fedha 2026/2027 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Amesema viongozi wanapaswa kuwa waangalifu wanapozungumzia masuala ya Muungano ili kulinda umoja na mshikamano wa Watanzania. Mbunge huyo pia amemuomba Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kuchukua hatua dhidi ya mawaziri na wabunge wanaodaiwa kutoa kauli zenye viashiria vya ubaguzi.

Jamii Voice
Jamii Voice
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 16 June 2026 09:38:33 GMT
3786
149
5
9

Music

Download

Comments

mahmoud.muya
Mahmoud Muya :
safi sana msukuma
2026-06-16 17:32:17
1
egarchatilagmail.c
Baba.JR@ :
respect
2026-06-16 16:42:23
0
emmanuelmseke746
Emmanuel Mseke :
kabisa tena wawakanye vijana wao wanaropoka sana
2026-06-16 10:14:47
2
2026antidi
2026-06-17 05:29:09
0
To see more videos from user @jamiivoice_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About