@jamiivoice_: Bungeni: Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma amekosoa utaratibu unaowalazimu madereva kurejea darasani na kufanya mitihani upya wanapokwenda kuhuisha leseni zao za udereva, akidai unadhoofisha nguvu kazi na kuathiri maisha ya familia zinazowategemea. Akichangia mjadala wa Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka wa fedha 2026/2027 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali, Musukuma amesema wafanyakazi wa sekta nyingine wanapopewa mafunzo hupata posho na kurejea kazini wakiwa na ari zaidi ya kazi. Amesema tofauti na hilo, madereva wanatakiwa kuhudhuria mafunzo kwa wiki kadhaa na kufanya mtihani ili kuhuisha leseni zao, hali inayoweza kuathiri ajira zao endapo watafeli. “Dereva ana watoto, familia inamtegemea na anaishi nyumba ya kupanga. Akifeli mtihani unamwambia arudi nyumbani akae, wakati hana kazi nyingine ya kufanya,” amesema Musukuma. Mbunge huyo amehoji pia mantiki ya kuwataka madereva wenye uzoefu wa muda mrefu na rekodi nzuri za usalama barabarani kurejea darasani. “Dereva ameendesha gari kwa miaka 30 bila historia ya ajali, bado unamwambia aende akasome,” amesema. Aidha, amesema utaratibu huo unasababisha baadhi ya kampuni na wamiliki wa magari kukosa madereva kwa wakati mmoja pale wanapokuwa wamepelekwa kwenye mafunzo, jambo ambalo linaathiri shughuli za kiuchumi.

Jamii Voice
Jamii Voice
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 16 June 2026 10:06:58 GMT
161635
8974
425
770

Music

Download

Comments

david69__0
David :
msukuma mda mwingine ana akil san 🤝👏
2026-06-16 11:52:25
109
user6253867442129
Tinkler madubansi .J. malema :
I am a driver from Zambia I support you big man for that request God bless you 🙏🙏🙏 and Tanzania drivers God bless you all
2026-06-16 13:50:00
54
ochuboyshaban
Ochu :
Respect 🫡 to you bro
2026-06-16 17:20:12
2
seiphmaugado
seiphmaugado :
mweshumiwa dereva
2026-06-16 13:38:10
32
mlulalucas
mlulalucas :
hata mpinzani anaipenda hii
2026-06-16 13:00:43
43
jonasjoseph9
jonasjoseph :
sana madereva tuna teseka mno
2026-06-16 15:49:32
19
tariq_1213
TARIQ :
Hoja nzuri sana
2026-06-16 15:45:13
12
ommary.chikwanda
Ommary Chikwanda Chikwanda :
kweli baba mungu akuondole Shari mbaya za Dunia akupe Shari zuri ya Dunia
2026-06-16 14:09:57
18
user82960281056572
tubwi98 :
mungu ametukumbuka madereva ubarikiwe sana msukuma.
2026-06-16 13:29:47
19
user8114362917485
user8114362917485 :
Ni sawa tunampongeza sana msukuma lakini je hayo mapendekezo yake yatafanyiwa kazi????
2026-06-16 15:16:10
16
nabii.camara
Nabii Camara :
Uyu jamaaa anaongea ukweli sana
2026-06-16 14:19:27
12
paulochamajibu
Paulo chamajibu kanyolo :
hapo umeongea ukwer kabisa msukuma
2026-06-16 12:06:50
12
mubahbrown
Mubah brown :
yani hii imekaa sana
2026-06-16 15:59:41
8
ralphdzy0
ralphdzy :
msukuma is very brighter
2026-06-16 17:39:52
2
benedict.luvanda
ben :
msukuma 100/100....ziwepo semina tu
2026-06-16 12:55:16
11
jenetmosh
mama ni mmoja :
Asante msukuma
2026-06-16 16:09:48
6
brave8882
Brave@888 :
critical thinker
2026-06-16 18:06:00
0
hajilukani7
Haji the Giant :
congratulations hoja za msingi mnoooo
2026-06-16 18:24:47
0
edomantz6
Edoman 🇹🇿AREA 5️⃣1️⃣ :
shida ya uyumsukuma anaongea point tu 🫡💯🙌
2026-06-16 16:30:52
5
shehe.abdalah
Shehe Abdalah :
dah hongera kwa kutufikishia ili jambo
2026-06-16 15:19:49
8
max.mwema
Max Mwema :
asante sana muheshimiwa kwa kutusemea sisi madereva wangepatikana wengine 50 kama ww
2026-06-16 15:39:55
11
mrsamaki11
vifaranga vya samaki bei poa :
huyu jamaa atunzwe saaana
2026-06-16 14:18:32
10
nelson.alphonce6
Nelson Alphonce :
yaan we msukuma hii point imenipa furaha
2026-06-16 13:12:01
11
loseryanslaa
Amani :
Asante kwa kupaza sauti kiukwel
2026-06-16 14:19:06
5
matoboymkuthe.sam
Matoboymkuthe samson :
hiii wasomi wanatuchelewesha saaana
2026-06-16 13:29:27
6
To see more videos from user @jamiivoice_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About