@chomozatv: Ushuhuda wa kugusa moyo wa Dada Tina ambaye alifika mahali pa kukata tamaa kabisa ya maisha. Kutokana na mzigo mkubwa wa matatizo, alimtafuta Mchungaji Eliona Kimaro na kumuomba amwombee afe kwa sababu aliona hakuna tena suluhisho. Mume wake alikuwa mgonjwa na akiendelea na vipimo vya uchunguzi (diagnosis), nyumba yao ilikuwa karibu kupigwa mnada na benki huku zikiwa zimebaki siku 14 tu waondolewe, na watoto wao walikuwa wamefukuzwa shule. Ilionekana kama majaribu yalikuwa yamezingira kila upande. Lakini Mama Tina hakumwacha Mungu. Katikati ya hali hiyo ngumu, aliendelea kumtumaini Mungu. Siku ambayo hakuitarajia, Mungu aliingilia kati na kubadilisha hali yote. Leo anasimama na kushuhudia ukuu, uaminifu na nguvu za Mungu katika maisha yake. Swali: Je, umewahi kufika mahali pa kukata tamaa kabisa lakini Mungu akabadilisha hali yako? Tuambie ushuhuda wako kwenye maoni hapo chini #2026Angaza #creatorsearchinsights