@paza_sauti_media: Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeandika historia mpya baada ya jopo la madaktari bingwa kufanikisha salama uzazi wa watoto watano kwa Bi. Victoria Mkwizu, mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam, katika tukio adimu la uzazi lililofanyika tarehe 13 Juni 2026. Watoto hao, watatu wa kiume na wawili wa kike, wamezaliwa wakiwa katika hali nzuri na wanaendelea kupatiwa uangalizi wa karibu huku hospitali hiyo ikiendelea kusimamia huduma bora kwa mama na watoto hao