@taimediatz: #HABARI Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, amewatolea uvivu wabunge Ester Bulaya na Ester Matiko, baada ya kuingilia hoja yake aliyoitoa kuhusu kodi na tozo watakazoenda kukumbana nazo wavuvi kwenye mwaka mpya wa bajeti. Ado amekataa taarifa iliyotolewa na Bulaya baada ya kutetea Chama cha Mapinduzi huku akihoji kuhusu umahiri wa CCM, Bulaya ameujua lini na kukataa wazi taarifa iliyotaka kutolewa na Mbunge Ester Matiko. ✍🏿 @mariamshabanitz #taimediatz #taimediatv