@novolaiza: Kamati ya Mahusiano ya Nje ya Seneti ya Marekani imepitisha muswada unaotaka kufanyika kwa tathmini ya kina ya uhusiano kati ya Marekani na Tanzania kufuatia kile kilichoelezwa kuwa ni ongezeko la matukio ya vurugu za kisiasa na kudorora kwa misingi ya demokrasia nchini Tanzania. Muswada huo wa pande mbili za kisiasa, ulioandaliwa na Seneta Jeanne Shaheen kwa kushirikiana na Seneta Ted Cruz, unaielekeza Serikali ya Marekani kufanya mapitio ya kina ya ushirikiano wake na Tanzania pamoja na kutathmini athari za mwenendo wa kisiasa wa nchi hiyo kwa maslahi ya Marekani katika Ukanda wa Afrika Mashariki.