@veriafya: Katika Mkutano unaoendelea Jijini Mbeya ukihusisha Chama cha Wataalamu wa Macho nchini, mojawapo ya Mjadala uliozungumzwa ni kuongezeka kwa Watu wenye Matatizo ya kupoteza Uoni wao, ikiwemo Watoto wadogo. Pamoja na mambo mengine, Wataalamu hao wamebainisha Matumizi ya Vifaa vya Kielektroniki kwa Watoto, hasa simu na tablet ni miongoni mwa visababishi vya kuongezeka kwa changamoto hii, kwani Wazazi wengi hutumia kama njia ya kuwatuliza.