@nashpointdesign: CHAIR WORKOUTS ๐ช Ni mazoezi ya kutumia kiti na rahisi sana kufanya, yanafaa kwa watu wa viwango tofauti kama wanene, wembamba au wa kati. Ni mazoezi yanayofanyika ukiwa umekaa au ukitumia kiti kama msaada na yaanafaa zaidi kwa: ๐๐ฝ Wanaoanza mazoezi ๐๐ฝ Wenye uzito mkubwa ๐๐ฝ Wazee ๐๐ฝ Wenye majeraha FAIDA ZA CHAIR WORKOUTS ๐ช ๐๐ฝ Huongeza nguvu za misuli kama mikononi, miguuni na tumboni. ๐๐ฝ Husaidia kuchoma mafuta hasa ukifanya kwa kasi ya juu. ๐๐ฝ Huboresha mzunguko wa damu. ๐๐ฝ Hupunguza hatari ya kuanguka hasa kwa wazee. ๐๐ฝ Ni salama na rahisi kufanya nyumbani au ofisini. ๐๐ฝ Hufanya mwili kuwa mwepesi na imara zaidi. Yapo mazoezi mengi yanayohusishwa na kiti lakini hii ni mifano midogo ya miongoni mwa mazoezi hayo: 1๏ธโฃ Seated Leg Raises (Kuinua miguu) ๐๐ฝ Kaa wima, nyoosha mguu mmoja juu ๐๐ฝ Shikilia sekunde 3โ5, kisha shusha ๐๐ฝ Rudia mara 10โ15 kwa kila mguu 2๏ธโฃ Chair Squats ๐๐ฝ Simama mbele ya kiti ๐๐ฝ Kaa taratibu kisha simama tena ๐๐ฝ Rudia mara 10โ15 3๏ธโฃ Seated Arm Circles ๐๐ฝ Nyosha mikono pembeni ๐๐ฝ Zungusha duara ndogo ๐๐ฝ Fanya sekunde 20โ30 4๏ธโฃ Seated Twists (Kwa tumbo) ๐๐ฝ Kaa wima, geuza mwili kulia na kushoto ๐๐ฝ Rudia mara 15โ20 Hapa tuna mazoezi 16 + 1 kwa ajili ya Body Stretching, haya yatakusaidia kuimarisha mwili na akili kwa ujumla๐ โฑ๏ธ Kila zoezi utakalofanya lina utaratibu, ratiba na mpangilio maalum. Mfano wa Ratiba hii fupi inaweza kukusaidia: ๐๐ฝ Dakika 5: Kupasha mwili moto (Warm Up) ๐๐ฝ Dakika 15-20: Mazoezi ya kiti (Chair Workouts) ๐๐ฝ Dakika 5: Kupunguza mwendo (Cool Down) ๐๐ฝ Unaweza pia kuhesabu 1-40 ili kupata dakika 1 ๐๐ฝ Fanya mara 3-5kwa wiki kwa matokeo mazuri. โ ๏ธ TAHADHARI ๐ Tumia kiti imara kisichoteleza ๐ Epuka kukunja mgongo kupita kiasi ๐ Anza polepole kama wewe ni beginner ๐ Kama una tatizo la kiafya, wasiliana na daktari โผ๏ธMUHIMU Kwenye safari ya kufanya mazoezi, fanya kwa ajili ya afya yako, kujenga akili yako na kubwa zaidi kujipenda kwako na usifanye kwa kushindana na mwingine.๐ โข โข TAG + SHARE + SHARE kwa mpendwa wako anayestahili kuona na kuwa miongoni mwa safari hii na kwa matumizi ya baadaye. For more tips @nashpointnutrifit
Nasra Nassor
Region: TZ
Friday 19 June 2026 21:08:28 GMT
Music
Download
Comments
Cutedidah :
Upo wapi tuwe tunafanya pamoja,๐๐๐ค
2026-06-20 06:00:28
1
To see more videos from user @nashpointdesign, please go to the Tikwm
homepage.