@nyayozamaulamaa: Naibu Kadhi Mkuu Sheikh Ally Ngeruko Aipongeza Familia ya Kiluwa Pamoja na Mahujaji Kwa Kitendo Kitukufu Walichofanya Naibu Kadhi mkuu ametoa pongezi hizo leo kwenye hafla ya Dua maluumu ya kumshukuru mungu kwa kurejea salama kwa mahujaji kutoka makkah kwenye ibada ya hijja iliyanyika katika ukumbi wa Serena Hotel iliyopo posta jijini Dar Es Salaam, Hafla hiyo imeandaliwa na Mfanyabiashara Mkubwa Bw. Mohammed Said Kiluwa Mkurugenzi wa Kiluwa Group na Kiluwa Steel Group na kuhudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri hapa nchini.