@wizara.ya.ardhi: MMUYA ATAKA WAMILIKI WA ARDHI KULIPA KODI YA PANGO LA ARDHI KWA WAKATI KUEPUKA RIBA YA ASILIMIA 1 Arusha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, ametoa wito kwa wamiliki wote wa ardhi nchini kuhakikisha wanalipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wakati ili kuepukana na faini na adhabu zisizo za lazima. Akizungumza leo, tarehe 20 Juni 2026, katika kikao kazi kilichowakutanisha wananchi wa Wilaya ya Arusha pamoja na wataalamu wa ardhi wa Mkoa wa Arusha kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo, Mhe. Mmuya amesisitiza kuwa serikali haitafanya mzaha na mtu yeyote atakayekiuka matakwa ya sheria hiyo. Mhe. Mmuya ameweka wazi kuwa kila Mtanzania anayemiliki ardhi kihalali ana wajibu wa kisheria kulipa Kodi ya Pango la Ardhi. Aidha, amewaonya wale wanaotumia kisingizio cha kutofahamu sheria ili kukwepa wajibu huo. "Kutokufahamu si kinga ya kutoadhibiwa. Sheria zetu zimeweka kipengele hiki wazi, na ukienda kinyume unaonekana ni mzembe tu. Sitaki niwaingize kwenye eneo hilo la kusema hamkufahamu," alisema Naibu Waziri Kaspar Mmuya. Naibu Waziri amefafanua utaratibu wa ulipaji wa kodi hiyo kwa mwaka wa fedha, akibainisha kuwa wamiliki wote wa ardhi wanatakiwa kulipa kodi zao ndani ya miezi sita ya kwanza ya mwaka wa fedha bila kuongezewa riba au faini yoyote. Hata hivyo, mmiliki yeyote ambaye atakuwa hajalipa kodi yake baada ya kipindi hicho ataingia rasmi katika hatua ya kutozwa penalti, ambapo atakatwa riba ya asilimia moja (1%) kila mwezi kulingana na kiasi anachodaiwa. Ili kuondoa malalamiko na mkanganyiko miongoni mwa wananchi, Mhe. Mmuya amebainisha kuwa vigezo vitatu vikuu vinavyotumika kupanga viwango vya Kodi ya Pango la Ardhi ni ukubwa wa eneo, matumizi ya ardhi pamoja na eneo ilipo ardhi husika (location).

WIZARA YA ARDHI
WIZARA YA ARDHI
Open In TikTok:
Region: TZ
Sunday 21 June 2026 13:52:00 GMT
162563
2619
345
1419

Music

Download

Comments

focusman63
focusman63 :
kodi nyingiii ila maendeleo sasa 0
2026-06-22 04:50:02
108
am_pseudocode
Ⓐ︎Ⓜ︎ :
Hii nchi njaa njaa sana
2026-06-21 19:21:06
49
vaydepretyvaydepr
vaydepretyvaydepr :
kwani kodi ya pango si inakatwa kwenye umeme?
2026-06-22 09:20:35
35
walikukunazi
walikukunazi :
Natamani kulipa ila na nyie mtupatie hati zetu mapema, tunasumbuka sana
2026-06-21 14:12:16
33
user4099126615887
St kitengo :
UKOLONI NI NINI???
2026-06-21 14:57:47
26
rahimaramdan953
rey :
silipi na hakuna kitu mtafanya
2026-06-22 06:42:58
13
temi47004
Temi :
kwa kutaka kodi tu hamjambo lakini kutupa hati ndio hamtaki. Tangu 2023 nimeprocess hati sijapata lakini natumiwa message za kulipa tu kodi
2026-06-22 11:16:25
13
malikiarecho
malikiarecho :
Ardh niya MUNGU au ni ya Nchi achen zenu MUNGU anawaona ,, basi daini na kodo ya Pumzi aliotoa MUNGU
2026-06-22 11:42:34
7
khadija.kmwaipaya
Khadija Kmwaipaya :
mm sijafaham kulipia jengo au ardhi
2026-06-22 18:27:29
3
papaa3324
papaa :
sasa hii ya umeme ni ya nn
2026-06-22 07:13:27
3
last_king_of_zamunda
BakaI :
tunalipaje kodi na hati zetu hamtoi.. mwaka umepita tangu niombe ila bila bila
2026-06-21 18:04:36
7
wondergloria123
wondergloria123 :
Nashukuru mie mlipaji mzuri sana
2026-06-22 04:51:38
3
saididdihewasi
side Dickies :
Ile tunaolipia tukilipa umeme ni kodi ya nini naomba kujuwa
2026-06-22 06:59:07
4
ruu01192
Ruu Kidoty🦋✈️ :
mwenye anajua taratibu za upatikanaji wa hati Aniambie jmn
2026-06-22 04:19:19
3
urocke23
urocke23 :
Sasa kulikuwa na maana gani ya kuwa na uhuru
2026-06-22 13:39:19
3
eliandosy2
elia ndosi ndosy :
duh karibu Tanzania Kila kitu ni kod. saiv mpaka kwenye mazao. yan. una Lima wew ata dawa awakuchangii ila wana taka ushuru. 🙌🥺
2026-06-22 10:31:35
1
www.barrick.com
engineer :
ukoloni maomboleo
2026-06-21 21:33:34
5
bamizat
BAMIZATZ :
unajiamulia sana bro
2026-06-22 07:51:55
1
sebastiangodian8
Sebastian Godian :
Kwani ardh ni ya serekali au ni ya nan mbn hii nch ni ya moto sana
2026-06-22 11:22:17
4
user7035851838335
smart boy 06 :
yule marehemu mungu amlaze mahala pema wallah pana tabu kupata tabu kukosa tabu
2026-06-22 14:48:10
2
maisha.plus7
maisha plus :
kuna kodi ya majengo kwa lazma tunalipa afu kuna kodi ya ardhi khaaa jamani 🥺🥺🥺
2026-06-22 06:34:57
4
matanmbo
Matambo :
Mimi bado sijaelewa kabisaa yaanii kabisaa
2026-06-22 13:11:52
1
lovenessmosha2
love mosha :
Sasa mtu amemilik arch toka mwaka 70 mzee hajui chochote leo anatumiwa taarifa anadaiwa kodi ya ardhi milion 7 kweli jaman
2026-06-24 06:41:57
1
user2790202137359
mamy :
Tunalipia wapi hii
2026-06-22 14:53:49
1
minaelmartin
Minael Martin :
mm silipi
2026-06-22 05:56:56
2
To see more videos from user @wizara.ya.ardhi, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About