@dr.saluh: Ilikuwa Mida ya saa kumi jioni. Mvua ilikuwa inanyesha nje. Hospitali ilikuwa imebaki kimya. Ndipo mwanaume mmoja akaingia. Ana miaka kama 38. Mwenye sura ya uchovu. Lakini aliyekuwa amevaa vizuri. Alikaa mbele yangu bila kusema neno. Mikono yake ilikuwa inatetemeka. Nikamuuliza: “Una shida gani kaka?” Akaweka karatasi mezani. Kisha akasema: “Doctor, nimepima sehemu fulani.” “Nimeambiwa kuna tatizo.” “Nimekuja urudie tena.” Nilimwangalia. Machoni alikuwa na hofu kubwa sana . Ile hofu ya mtu ambaye moyo wake tayari unajua ukweli lakini akili yake inakataa kuukubali. Nikachukua sample ya Damu nikaenda kupima . Tukawa tunasubiri majibu . Dakika zilikuwa zinaenda. Muda wote alikuwa anaangalia simu yake. Mara nikamuona akitabasamu. Nikamuuliza: “Unaangalia nini?” Akageuza simu. Akaniambia: “Hawa ndiyo watoto wangu.” Kwenye picha kulikuwa na watoto watatu. Mmoja alikuwa amebebwa mabegani mwake. Wote walikuwa wanacheka. Kisha akanionyesha picha nyingine. Mke wake. Akasema: “Doctor, huyu mwanamke amenivumilia miaka 14.” “Nilikuwa sina kitu.” “Leo tunaishi vizuri kidogo kwa sababu yake.” Nilinyamaza. Kwa sababu muda huo matokeo yalikuwa tayari mbele yangu. Na moyo wangu ulikuwa mzito. Nilitazama matokeo kwa sekunde kadhaa. Kisha nikainua macho nikamtazama. Yeye alikuwa bado anatabasamu kidogo. Hakujua nilichokuwa nakiona. Akaniuliza: “Doctor, kuna shida?” Nikavuta pumzi ndefu. Nikamwambia: “Tunahitaji kufanya kipimo kingine cha uthibitisho. (UN-GoLD )” Tabasamu lake likapotea. “Kwa nini?” “Ni utaratibu tu.” Lakini ukweli ni kwamba tayari moyo wangu ulikuwa mzito. Dakika chache baadaye nikachukua sample nyingine. Chumba kikawa kimya. Ukimya wa kufikirisha. Hakukuwa tena na mazungumzo ya kawaida. Kulikuwa na sauti ya saa ukutani tu. Tik… Tak… Tik… Tak… Jamaa alikuwa amekaa akiwa ameshika simu yake. Mara kwa mara akiangalia picha za watoto wake. Dakika zilikuwa zinaenda . Hatimaye matokeo ya uthibitisho yakaanza kuonekana. Mstari wa kwanza ukatokea. Kisha wa pili. Nilihisi moyo wangu unauma sana . Kwa sababu nilijua sasa hakukuwa na mashaka tena. Nikakaa kimya kwa sekunde kadhaa. Yeye akanitazama. Kisha akauliza kwa sauti ya chini: “Doctor…” “Mbona huongei?” Nikaweka kifaa mezani . Nikamuomba akae. Alipoona uso wangu… tabasamu lake likapotea. Nikaanza kuzungumza kwa utulivu. Kadri nilivyoendelea… uso wake ukabadilika. Akanitazama. Akatazama kipimo. Kisha akasema: “Hapana.” Nikanyamaza. Akaendelea: “Hapana doctor.” “Rudia tena.” Nikajaribu kumueleza. Lakini hakusikia. Akasema tena: “Rudia tena.” “Labda safari hii kitakosea.” Nikamwambia tayari tumerudia hapo na matokeo ni Yale Yale kaka .. hakusema kitu. Alibaki kimya. Kimya cha kutisha. Kisha akauliza swali moja. Swali ambalo mpaka leo silijasahau. “Doctor…” “Ni kwa namna gani nitamuagalia mke wangu usoni leo?” Machozi yakaanza kumtoka. Akaendelea. “Ni vipi nitamwangalia mtoto wangu wa kwanza?” “Ni vipi nitamkumbatia mwanangu wa mwisho?” “Mimi nilikuwa nataka tu kuwa baba mzuri.” Kisha akainamisha uso wake. Akalia. Sio kilio cha ugonjwa. Sio kilio cha kifo. Ilikuwa ni kilio cha mtu aliyekuwa anaogopa kuvunja mioyo ya watu aliowapenda zaidi duniani. Kabla hajaondoka… Alisimama taratibu. Akafuta machozi yake. Akachukua simu yake. Akaifungua. Kulikuwa na picha ya mke wake na watoto wake watatu. Wote walikuwa wanacheka. Wote walikuwa na furaha. Wote walikuwa wanamsubiri arudi nyumbani. Alitazama picha ile kwa muda mrefu. Kisha akaniuliza swali moja ambalo mpaka leo sijawahi kulisahau. “Doctor… nikifika nyumbani leo, nianze kumwambia mke wangu ukweli au nimkumbatie kwanza?” Sikuweza kujibu. Kwa sababu wakati mwingine hakuna shule inayokufundisha kujibu maswali ya aina hiyo. 💔 #swahilitiktok #tiktoktanzania🇹🇿 #viraltiktok #hiv #ukimwi
ila wewe uloo Andika hii stori umesomea pia ujasahau hata sentence 1 nimeipenda sana
2026-06-23 20:29:59
310
Popo masta.2 :
Ambao Tunampenda MUNGU gonga like ❤️natuurmens ahsante MUNGU🙏🙏🙏
2026-07-10 18:47:48
164
Mwadawa Mpoto :
pole sana mungu akupe nguvu maisha yasonge
2026-06-23 07:09:17
64
faubryden :
hee mungu tunaomb utusaidieh sis vijana wako na utulinde mungu wetu
2026-07-06 10:27:13
34
Tatu Mtevu :
kuomba mungu2 mana halina mmoja ata ukutulia mwenzio atakuletea
2026-07-22 07:01:07
28
lucy love :
me sijaelewa chochote kuhusu hii story 😳
2026-07-20 20:22:00
5
Ester john277 jr :
Nimelia 😭😭😭japo ndio naina leo trh15 mwz 7 ila ili jambo lickie kwa mwenzako cjui nilini MUNGU atamponya mume wangu na pepo la umalaya
2026-07-15 14:08:17
6
Ibraah Baraka :
mungu amtie nguvu
2026-06-30 11:16:40
13
@fee ness :
Mungu tunaomba ututetee na utulinde piaa hakupenda awe hvy🥺
2026-07-03 16:06:42
25
saida :
Allah atujalie mwisho mwema
2026-07-08 15:51:18
8
Simb@ mp0le👉👈 :
mungu awalindeje tuache uzinzi
2026-07-04 16:11:51
8
MoodyAthu@ :
mhhhh Pole.sana na mungu ampe nguvu mahala alipo
2026-07-09 17:47:10
12
Charlse&Eksa tz :
ambao hatujaelew like hap
2026-07-03 11:14:53
25
user1116638754029 :
pole sana m. mungu akutie nguvu katika hili
2026-07-07 20:00:58
9
niffer :
allah atujalie mwisho mwema 🙏
2026-07-02 17:05:26
9
Agness Sangana💞🌹 :
MUNGu amsaidie sana Kila jambo Lina wakati wake wakati wa MUNGu ni wakati sahihi🙏🙏 m nimeumia sana lakini naamini ipo siku atafurahi sana kwa maajabu ya MUNGu🙏🙏🙏🙏
2026-06-23 12:08:46
86
pizzo kidy🎤🎵 :
mimi natafuta like huku tik tok
2026-06-26 16:55:46
16
‿⃪ᷝ ⷨ—͟͞͞★𝐌𝐎𝐇'𝐃.𒁍 :
dah allah ampe nguvu na mungu atunusuru
2026-06-23 07:51:16
24
Eles Kilipamwambu :
mungu akurindie familiar yako
2026-06-23 06:27:19
30
To see more videos from user @dr.saluh, please go to the Tikwm
homepage.