@momadini_: Maumivu si mwisho wa safari, ni sehemu ya safari. Mwanaume atalia, atachoka, atasalitiwa, atapoteza, na wakati mwingine ataanguka. Lakini hayo yote hayamfanyi ashindwe. Kushindwa huanza pale anapoamua kubaki chini, kuishi kwenye kumbukumbu za jana na kuacha kupigania kesho. Endelea kutembea. Hata hatua ndogo bado ni hatua ya mbele. Mwanaume hashindwi na Maumivu. #MoMadini #creatorsearchinsights #fpy #motivation #unanitazamausoniunapatapicha