@bantu_media: Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Prof. Mussa Assad, amesema ni muhimu kuwepo kwa utaratibu wa ukaguzi na ufuatiliaji wa maisha ya viongozi wa umma wanaoteuliwa kushika nafasi mbalimbali serikalini. Prof. Assad amesema tathmini hiyo haipaswi kufanyika kwa viongozi pekee, bali pia kuwahusisha ndugu na watu wa karibu wanaoweza kuhusishwa na mali au shughuli zao za kiuchumi, ili kuweka wazi suala la uadilifu na uhalali wa umiliki wa mali. Akizungumza katika mahojiano na Clouds TV, Prof. Assad amesema ukaguzi huo wa mara kwa mara unaweza kusaidia kubaini mwenendo wa maisha ya viongozi na kutoa taswira ya namna mali wanazomiliki zinavyopatikana wakati wa kipindi chao cha uongozi. Ametoa mfano wa kiongozi mmoja anayemfahamu ambaye, ndani ya kipindi cha miaka mitano akiwa Waziri, ameweza kumiliki magari ya kifahari ikiwemo magari matatu aina ya Land Cruiser LC 300 pamoja na Range Rover, huku akiishi maisha ya gharama. Kwa mujibu wa Prof. Assad, hali hiyo inaleta maswali kuhusu namna mali hizo zilivyopatikana ndani ya muda mfupi na umuhimu wa kuwa na mifumo madhubuti ya uwajibikaji kwa viongozi wa umma. Amesisitiza kuwa uwazi, uadilifu na ufuatiliaji wa mali za viongozi ni hatua muhimu katika kujenga imani ya wananchi na kuhakikisha viongozi wanawajibika kwa nafasi wanazopewa. CC: CLOUDS MEDIA
Bantu Media
Region: TZ
Tuesday 23 June 2026 08:32:52 GMT
Music
Download
Comments
Salim Mansoor :
watu kama Hawa walioonyoka hawatakiwi kabisa ila MUNGU ndio anawalinda Salut sana kwake professor
2026-06-25 03:24:31
15
cleartzboy :
professor asaad simba uyu
2026-06-25 19:12:17
4
Janekay :
Am so interested to listen to this man.Yupo smart sana
2026-06-24 21:33:00
6
KessyLug :
Lifestyle Audit📌
2026-06-23 18:19:54
6
mfaumesulleiman :
upo Sawa professor
2026-06-25 11:21:58
3
jumaothmani :
Yupo sawa huyo Mwamba
2026-06-25 01:55:05
5
user2327842304405 :
boss unafaa kabisa kuwa Rais
2026-06-27 14:11:52
2
Peter Tarimo :
fact
2026-06-23 16:26:33
3
... :
$1billion😳
2026-06-26 12:20:51
0
Yusuf Sella :
Mzee yupo Sahihi
2026-06-27 13:25:51
0
Ally Omary :
huyu yuko sahihi sana
2026-06-25 17:47:32
1
Homoud jr :
swadakta
2026-06-24 08:25:15
1
CHUSSE JR :
ni sahihi
2026-06-23 20:03:32
2
benja_ kuku_ madini tz👆 :
fact
2026-06-23 12:18:23
3
MTENGWA. :
Namkubali sana huyu mwamba
2026-06-23 12:31:52
8
RashidMashaka :
fact
2026-06-23 09:42:07
3
Babuu :
maana ya muislamu swafi
2026-06-24 04:15:58
5
evans tech :
iyo kitu awawez kubal iwepo waiz niweng sana
2026-06-25 03:11:36
1
saidmohammed1780 :
nakukubali mzee ..you are true professor ...not professor lipumba
2026-06-25 13:59:11
0
laizare3 :
Wizi tu
2026-06-26 08:13:24
0
dotto mtoro :
Hio ni nzuri sana ila itapigwa vita hatari kwenye nchi hii
2026-06-23 11:29:10
1
hatunaga namba AD :
nimwendo wakuibatu
2026-06-25 04:10:05
0
SīDē👊🏾5 :
🙏🙏🙏🙏🙏🙏
2026-06-23 09:48:48
0
allyjux696 :
🤔🤔🤔
2026-06-28 08:32:05
0
To see more videos from user @bantu_media, please go to the Tikwm
homepage.