@uzunguni_city_park: Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutambua na kuthamini mchango wa sekta binafsi na wawekezaji katika maendeleo ya taifa. Pia tunatoa shukrani za pekee kwa Kamati ya Mwenge wa Uhuru, viongozi wa Wilaya ya Korogwe, pamoja na Waheshimiwa Wabunge wa Korogwe kwa kutuamini na kuichagua Uzunguni City Park Korogwe kama moja ya taasisi zinazotoa huduma bora kwa jamii. Tunajivunia heshima ya kuwekewa jiwe la msingi na tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa maendeleo ya Korogwe na Tanzania kwa ujumla. Asanteni sana kwa imani yenu kwetu🙏🏽🇹🇿