@alnadhifislamic: Linda Usafi wa Moyo Wako: Usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa ni muda wa baraka. Jiepushe kabisa na mambo yanayoweza kupiga doa jeusi kwenye moyo wako usiku huo (kama kuangalia mambo yasiyofaa kwenye simu au kusengenya). Ukiingia Ijumaa ukiwa na moyo msafi, utapata utulivu mkubwa wa kufanya ibada. Kithirisha Swala kwa Mtume (ﷺ): Usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa ndio muda bora zaidi wa kumwombea rehema na amani kiongozi wetu (ﷺ). Mtume amesema: "Kithirisheni kuniswalia siku ya Ijumaa na usiku wake." Kila swala moja, Mungu anakurehemu mara kumi. Wahi Kusoma Surat Al-Kahf: Usisubiri mpaka Ijumaa mchana ukiwa na haraka au majukumu. Unaweza kuanza kusoma nusu ya surah hii tangu Alhamisi usiku baada ya Isha ili kuivuta ile nuru itakayokuangazia wiki nzima. Jipange Kuwahi Rakah ya Ijumaa: Maandalizi ya mapema tangu Alhamisi usiku yanakusaidia kutochelewa swala kesho yake. Mtume (ﷺ) ametupa mwongozo muhimu sana akisema: "Mwenye kuwahi rakah moja ya Swala ya Ijumaa, basi amewahi Swala hiyo (yaani atahesabika amepata thawabu za Ijumaa). #islamicquotes #islamic #islamic_video #islam #islamicreminder

AL NADHIF ✨
AL NADHIF ✨
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 25 June 2026 07:04:39 GMT
4226
552
2
21

Music

Download

Comments

ashrayyah
ashrayyah :
Allah tujaalie kuwa wenye kupata barka hizo 🤲🤲
2026-06-25 13:24:23
3
To see more videos from user @alnadhifislamic, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About