@saut.digital: Makamu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Padri Prof. Juvenalis AsanteMungu, amewataka wanafunzi na vijana nchini kuchangamkia matumizi ya teknolojia ya kisasa ili kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya utalii. Ametoa kauli hiyo katika Tamasha la Utalii la SAUT 2026 mkoani Mwanza, ambapo amesisitiza mkakati wa chuo hicho kuendelea kuwajengea uwezo wanafunzi kutumia zana za kiteknolojia katika sekta ya utalii nchini #SAUTDIGITAL #sautrending #radiosautfm #sautdigitalupdates #sautdigitalhabari