@hussain.ahmed2959:

Hussain Ahmed
Hussain Ahmed
Open In TikTok:
Region: BD
Sunday 28 June 2026 08:55:16 GMT
61
1
0
0

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @hussain.ahmed2959, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos

Kipindi cha ukoloni wa Wajerumani Njia za reli za kwanza Tanganyika, ikijulikana kipindi hicho kama Ujerumani Afrika Mashariki, zilijengwa mara  tu baada ya reli ya kwanza huko Zanzibar. Mwaka 1891 Eisenbahngesellschaft für Deutsch-Ostafrika (Kampuni ya Reli ya Ujerumani Afrika Mashariki) ilianzishwa, ikiwa na lengo la kujenga njia ya reli kutoka Tanga, Tanganyika kuelekea Bara. Kwa ajili hiyo, na baadaye, njia kuu katika koloni la Ujerumani, geji iliyochaguliwa ilikuwa  mm 1,000 (futi 3 kwa inchi 3 3/8) mita geji.  Kwa kuongeza, reli nyepesi zilijengwa Tanganyika mahususi kwa ajili ya mashamba ya mkonge zenye geji nyembamba, kwa kawaida geji 600 mm (futi 1 kwa inchi 11 5/8) Ujenzi wa Reli ya Usambara kutoka Tanga kuelekea Bara, ulianza mwaka 1893. Hata hivyo, kumpuni iliyokuwa inajenga reli hiyo ilifilisika baada ya miaka miwili. Kwa kipindi hicho, km 40 (maili 25) ya reli ndizo zilizokuwa zimekamilika, hadi kufikia Korogwe. Hazina ya mkoloni ilichukuwa mradi mwaka 1899. Miaka minne baadaye, mwaka 1903, ilitoa maelekezo kwa ajili ya kuendeleza ujenzi. Baadaye, kulikuwa na majaribio mengine kuendesha reli katika hali imara kiuchumi na kisheria. Mwaka 1904, reli ndogo ziliboreshwa. Wakati huo huo, nchini Ujerumani Kampuni ya Reli ya Sigi (Sigi-Eisenbahngesellschaft) ilianzishwa, ikiwa na lengo la kujenga reli nyembamba  kutoka Reli ya Usambara, yaani Sigi-Bahn katika geji ya mm 750 (futi 2 kwa inchi 5 1/2).  Mwaka huo huo, 1904 kampuni ya Reli ya Afrika Mashariki (Ostafrikanische Eisenbahngesellschaft (OAEG)) ilianzishwa  kusaidia reli kutoka Dar es Salaam kuelekea Ziwa Tanganyika, yaani Reli/Njia ya Kati (Zentralbahn). Kigoma ilifikiwa februari 2, 1914, mwanzoni mwa vita vya kwanza vya Dunia. Baadaye  mwaka 1914, kazi ilianzia Ruandabahn, njia kutoka Tabora katika ngome iliyokuja kuwa Rwanda. Mradi huu ulikwamishwa na kuzuka kwa Vita vya Kwanza vya Dunia. #TumetokaMbali #tanzania #sgr #tanganyika

About