@wepesitv: Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju amekemea vikali vitendo vya baadhi ya Viongozi wa Serikali na wa Kisiasa kuingilia utendaji wa shughuli za Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mahakama kwa kisingizio kwamba wao ni Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya. Mhe. Masaju ameyasema hayo tarehe 30 Juni, 2026 alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mahakama Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. “Hizo sheria zinazowapa madaraka hazikuwapa mamlaka ya kuingilia utekelezaji wa amri na maamuzi ya Mahakama. Wachukulieni hatua. Haiwezekani Mahakama imeshatoa amri halafu mtu mwingine anazuia, hiyo inakuwa ni Mahakama au ni kitu gani? Ni lazima tutofautishe shughuli za kisiasa na shughuli za kutoa haki zinazofanywa na Mahakama,” amesema Jaji Mkuu. Akizungumzia kuhusu Changamoto na Usimamizi wa Sheria, Jaji Mkuu amewaeleza, Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mahakama kuwa nao wana changamoto ndio maana wanaruhusu wanasiasa kuingilia utendaji kazi wao bila kuwachukulia hatua. “Hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria na hata mimi Jaji Mkuu siko juu ya sheria. Na kwanza hata mimi kwa kiapo changu na Majaji wote hapa na Mahakimu wote, na hata Wasajili tunaapa tunapotekeleza majukumu yetu kuzingatia Katiba, mila na desturi, na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bila hofu, upendeleo, wala chuki,” amesema Mhe. Masaju. Aidha, Jaji Mkuu amewataka Madalali na Wanasheria wao kuchukua hatua kali za kisheria, ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kinyume cha sheria (false imprisonment) au uzuiaji wa utekelezaji wa amri halali, Maofisa wa Polisi au Viongozi wanaokiuka Sheria kwa majina yao binafsi, kwani Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameshafafanua kuwa wavunja Sheria watagharamia makosa yao wenyewe.
WEPESI TV
Region: TZ
Wednesday 01 July 2026 14:02:40 GMT
Music
Download
Comments
Daz :
sure
2026-07-01 18:33:41
0
Happifanus :
Aiseee
2026-07-01 19:10:38
0
Sharifu Dadi :
good the boss
2026-07-01 18:39:50
0
Arnold Kimaro :
Absolutely.
2026-07-01 18:42:04
0
WA ADAM NA HAWWA(EVA) :
Bravo HAKI JAJI MKUU
2026-07-01 19:14:32
0
jmalle :
Vipi kesi ya Lisu
2026-07-01 18:05:10
0
Daniel Otieno :
bwana shemeji uko vizuri mungu asimame nawe
2026-07-01 17:48:25
0
Nyamgarama Mang'aba :
uko vizr mzee wangu hamna jita mzembe
2026-07-01 15:40:01
0
sfaf2024 :
WELL SAID 🙏
2026-07-01 18:11:42
0
traves :
kamdomo
2026-07-01 19:13:54
0
user9801221031581 :
Yani ninavo kuombea mungu Yani huna konakona ata saa moja
2026-07-01 18:22:16
0
goodluckisaya783 :
ni kutoka moyoniii?au cjui Niko wapi
2026-07-01 18:34:13
0
Peace Abesiga :
👏👏👏👏
2026-07-01 18:06:33
0
kimbwandaissa :
🔥🔥🔥🔥
2026-07-01 18:08:33
0
To see more videos from user @wepesitv, please go to the Tikwm
homepage.