@mshindo_tv: Mapema leo 01 Julai 2026 Baraza la Sanaa Sensa na Filamu BSSF Zanzibar lasitisha shughuli za upigaji wa muziki wa (Rusha roho) mitaani. Tamko hilo limetolewa mara baada ya kusambaa video mjongeo katika mitandao ya kijamii ikiwaonesha vijana wakicheza kinyume na maadili huku wakiwa wameshikilia mapanga, jambo ambalo ni hatarishi kwao na kwa wananchi wengine. Hapa Katibu Mtendaji wa baraza la Sanaa Juma Chum Juma anaeleza kuhusu Taarifa ya tamko hilo..... Kwa habari na matukio mbali mbali tufuatilie kupitia mitandao yetu #Mshindo tv.