@realabuzooh140: 1️⃣ Acha kumtafuta mtu asiyekutafuta. 2️⃣ Acha kubembeleza watu wengine. 3️⃣ Acha kuongea maneno mengi zaidi ya yale yanayohitajika. 4️⃣ Watu wanapokuvunjia heshima, wakabili hapo hapo mara moja. 5️⃣ Usile chakula cha watu wengine kuliko wanavyokula cha kwako. 6️⃣ Punguza mara ngapi unatembelea baadhi ya watu, hasa kama nao hawakutembelei. 7️⃣ Wekeza kwako mwenyewe na jifanye uwe na furaha. 8️⃣ Acha kushadidia au kusikiliza mambo ya umbea kuhusu watu wengine. 9️⃣ Fikiri kabla ya kuongea; asilimia 80 ya jinsi watu wanavyokuthamini inatokana na kile kinachotoka kinywani mwako. 🔟 Wakati wote pendeza/onekana vizuri; vaa vile unavyotaka kuheshimiwa na kuchukuliwa na watu. Tukue pamoja✊️✊️ #swahilitiktok #contentcreator #read #brotobro