@mzrh_tv: DKT. MBWANJI ASISITIZA UMOJA NA AFYA BORA KUPITIA TAMASHA LA MICHEZO NA VIPAJI JIJINI MBEYA Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH), Dkt. Godlove Mbwanji, leo amefungua msimu wa tatu wa Tamasha la Michezo na Vipaji la MZRH 2026 katika Viwanja vya Sokoine jijini Mbeya. Tamasha hilo linalotarajiwa kudumu kwa muda wa wiki moja, linajumuisha zaidi ya watumishi 1,200 kutoka idara na vitengo mbalimbali vya hospitali linahusisha mashindano katika michezo na vipaji mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguu, Mpira wa pete (Netiboli), Kuvuta kamba, Vipaji vya kuchora, Vipaji vya kuimba na Mengineo. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Dkt. Mbwanji amesisitiza umuhimu wa watumishi kushiriki katika michezo mbalimbali iliyoandaliwa kuimarisha utendaji kazi na afya za watumishi: "Kufahamiana eneo la kazi kwa watumishi wote inaweza isiwe rahisi, lakini kupitia michezo tunaweza kufahamiana zaidi. Michezo inatufanya kuwa familia moja na kuishi kama familia hivyo kila mmoja ashiriki kikamilifu. Sisi tunafanya kazi na kufurahia maisha." Kama sehemu ya motisha na kusherehekea ufunguzi huo, Uongozi wa hospitali umetoa supu na nyama choma kwa washiriki wote waliokuwepo viwanjani.
Mbeya Zonal Referral Hospital
Region: TZ
Wednesday 01 July 2026 19:31:17 GMT
Music
Download
Comments
mariam :
michezo kwa afya bora🙌🏻
2026-07-02 08:48:42
1
Aneth Bashiri :
our leader MUNGU Akulinde sana kiongoz wetu❤
2026-07-02 04:28:14
1
veronica :
mungu aendelee kukubariki na kukulinda kiongozi wetu
2026-07-01 20:02:59
1
To see more videos from user @mzrh_tv, please go to the Tikwm
homepage.