@kuku_dodoma_theresa: Mambo ya kujiandaa unapotarajia kupokea vifaranga kipindi hiki cha baridi kali Jambo 1.Ongeza bajeti ya kuwapa vifaranga joto mara 2 mpaka 4 ya Ile uliyoizoea, kwanini? Moja:Kuongezeka kwa kipindi unachotakiwa kuwapa vifaranga joto, kwa kawaida labda ulikuwa unawapa joto mpaka siku 8-10 unaishia hapo ila kwasasa unaweza kulazimika kuwapa joto mpaka siku 21 hasa usiku kuanzia saa 4/5 mpaka saa 4 asubuhi Mbili: Kuongezeka kwa jitihada inayotakiwa ili uweze kufikia joto sahihi kwa vifaranga kwasababu ya baridi kali utalazimika kuongeza vyungu au bulb bandani ili uweze kufikia joto wanalohitaji vifaranga mf siku 1 ni nyuzi joto 30-35 Wakati wa joto unaweza kuwa na vyungu 2 vikatosha kuwapa joto vifaranga 200 lakini wakati wa baridi kali ukalazimika kuwa na vyungu 4 Jambo 2: Katika kipindi cha baridi kali kunakuwa na magonjwa ya mara kwa mara hasa ya mfumo wa hewa kama mafua Kwahiyo kuwa makini kuwakagua kuku wako Jambo 3: Kama Jambo la kwanza na la pili halijazingatiwa kutakuwa na ulaji hafifu wa chakula utakaokuletea matatizo ya miguu na Vifo vingi vya vifaranga Jambo 4: Fuatilia kwa karibu ulaji wa chakula kwa vifaranga kama hawali chakula vizuri Hilo ni tatizo kubwa sana TAHADHARI ⚡ ☠️ VIFO VINGI SANA VITATOKEA JOTO LIKIWA CHINI NA VIFARANGA WANA MAFUA KWASABABU VIFARANGA WATABANANA ILI WAPATE JOTO NA KUSHINDWA KUPUMUA VIZURI KWASABABU YA MAFUA WAKATI HUO WATAKUWEPO AMBAO HAWAWEZI KUSIMAMA HAO WATAKUWA WA KWANZA KWASABABU WATAKANYAGWA ☎️☎️0752-396249

Kuku_dodoma_tee
Kuku_dodoma_tee
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 02 July 2026 14:32:16 GMT
1018
27
0
2

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @kuku_dodoma_theresa, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About