@akhi_ali5: Ijumaa ya leo, Tunakuomba ewe Mola wetu, usiziache nyoyo zetu zibebwe na huzuni, wala roho zetu zishindwe na majaribu. Pale tulipochoka, tupe nguvu. Pale tulipokata tamaa, tufufulie matumaini. Pale milango ilipofungwa mbele yetu, tufungulie milango ambayo hakuna awezaye kuifunga. Tufanye tuwe miongoni mwa wale wanaokutegemea kwa moyo wa dhati na wanaorejea Kwako katika kila hali. Hakika Wewe ndiye Mbora wa kusikia dua na Mbora wa kujibu. Aamiin Yaa Rabbal 'Aalamiin. 🤲 #creatorsearchinsights #viralvideo #jummamubarak