@pastor_kagoro_01: •📌 Wahubiri wengi wamesahau kuhubiri jinsi shetani anatumia Lango la Pua kuharibu nafsi za wana wa Mungu. Katika uumbaji, Bwana Yesu alitumia Pua kama Lango kupitisha pumzi ya Uhai na Leo kwa pua zetu huwa tunavuta hewa ya oxygen na tunaishi. Imeandikwa Mwanzo 2:7 [7]BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. •📌 Shetani akitaka kuharibu nafsi ya mtu husababisha watu kuvuta pumzi za mauti mfano harufu ya Moshi wa sigara au harufu ya Pombe na Vileo vingine. Mtu anapokuwa anavuta kwa pua harufu hizi huwa ananajisika na ndio maana ni muhimu kujitenga na maeneo na watu Wanaotumia Sigara na pombe kwa sababu wanakushirikisha dhambi zao. Imeandikwa Ufunuo wa Yohana 18:4 [4]Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. 📌• Unapokaa karibu na mtu anavuta Sigara au anakunywa pombe na ukanusa harufu yake ujue anakushirikisha dhambi yake na utapaswa kutubu kama mlevi au mvuta sigara na kujitakasa kwa damu ya Yesu Kristo. 📌NAMNA PERFUMES ZINATENGENEZWA Katika Biblia tunaona matumizi ya Manukato katika Agano Jipya na Agano la kale, lakini tatizo linaanza hapa, Perfumes zinatengenezwa kutoka kuzimu moja kwa moja na kuletwa duniani kwa ajili ya Kutumiwa na watu Wasio kuwa na utambuzi wa ROHO MTAKATIFU au katika Dunia, Kuna viwanda vinatengeneza perfumes hizi, wamiliki wa viwanda hivi ambao ni waabudu Shetani, huwa wanatamkia maneno ya laana bidhaa hizi za perfumes na kuziweka wakfu kwa shetani kwa Kafara na bidhaa hizi zinakuwa na maagano mabaya ya Shetani na huwa ni Mali za shetani huwezi kuzitakasa kwa Damu ya Yesu Kristo kwa sababu vimewekwa wakfu kwa shetani. 📌•Ukiangalia logo za perfumes na majina ya perfumes utaona zimebeba majina ya Shetani na picha zinazoonesha ufalme wa Bahari. Hii ni hatari sana. Imeandikwa Isaya 3:24 [24]Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri. 📌• unapojipulizia perfumes au unapokuwa unanusa perfume aliyojipulizia Mtu mwingine , ile harufu ya perfumes unapoinusa inaingia kwenye pua yako, ile harufu huwa inaingia kwenye nafsi yako na kutengeneza vidonda na baadae uvundo na nafsi yako inaharibiwa na Unapoteza Nuru ya utukufu wa Mungu ndani yako. Hii ni sawa na mtu anapokuwa anavuta harufu ya Moshi ya Sigara. Harufu ya perfumes ni pumzi ya mauti ya Shetani kuharibu nafsi ya mtu na kumnajisi kwa sababu bidhaa za perfumes ni Mali ya malkia Yezebeli. Mkristo Anapotumia perfumes anakuwa anaingia Agano na Yezebeli na kuuza nafsi yake kwa shetani Imeandikwa Ufunuo wa Yohana 2:20 [20]Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. •📌 perfumes zimebeba harufu zenye nguvu za kishetani ambazo huamsha tamaa ya ngono kwa watu wanapozinusa. Kuna harufu ya perfumes ukiinusa unaanza kumtamani kingono aliyejipulizia ile perfumes. Kwa sababu nyuma perfumes Kuna nguvu za kishetani za kumtongoza mtu anapoivuta katika mianzi ya Pua. Watu wengi wanaanguka kwenye uasherati au uzinzi kutokana na perfumes. Perfumes ni silaha ya Shetani kueneza uzinzi na uasherati katika Dunia hii. Imeandikwa Mathayo 5:28 [28]lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. •📌 Kuna perfumes wanawake wanatumia akipita karibu yako lazima ugeuke umtazame na umwangalie ni nani na badae unaanguka kwa kumtamani kwa sababu harufu ya perfumes imebeba nguvu za kishetani za kumtongoza mtu anapoivuta katika uasherati au uzinzi. 📌• Bidhaa za perfumes zimeunganishwa majina ya mabaha. Mtu Anapotumia perfumes anakuwa anajiambatanisha na majini na mahaba na ndio maana watu wanaota wanafanya ngono kwenye ndoto zao. #UKWELIHALISI
PASTOR JOHN KAGORO
Region: KE
Friday 03 July 2026 08:00:59 GMT
Music
Download
Comments
Dinah Mlekwa :
Vipi kuhusu marashi aliyopakwa Yesu na Mariam Magdalena?
2026-07-23 05:07:16
18
yong lady🤏 :
na watumishi wanatumia simu kufikishaujumbe hawatauona ufalme wa MUNGU
2026-08-14 19:28:31
2
Angel 😇 (◕ᴗ◕✿)🩷 :
Um what verse says this 😳
2026-09-06 16:28:46
0
kei george :
kupaka pafiumu siyo zambi ila kuna baadhi za pafiumu zinatoka kuzimu na kuna baadhi za pafiumu zinavutia majini mahaba sasa ili ujikinge na hayo yote unatakiwa kumuomba Mungu ili zile roho ambazozinakaa ndani yake zipate kuondoka ili zisijekukuingilia ww kwa kupitia pafiumu
2026-07-30 18:50:16
3
Mungu ni mwema :
Dah Mungu tutie nguvu yani mambo yamekuwa mengi mpk kichwa kinauma tutaponea wapi kila kitu sasa nitabu uwii hii mbingu ninjia nyembaba kumbe hapa sasa naelewa uwii Bwana Yesu turehem
2026-08-01 21:12:55
2
Patrick homes experts :
Mimi najiuliza namna gani hata nikinunua perfume nashindwa kutumia
2026-08-20 18:57:59
0
G-BOY BIG BOY :
tumekuelewa mzee sisi mbingu tunaitaka so tutaacha kila kitu tupat Mbingu
2026-07-25 14:49:22
0
baby j :
Mchungaj naomb kjuwa kuvaa miwani ni dhambi pia??????
2026-07-31 07:24:05
0
Jenipher :
i blv in it
2026-07-11 21:02:23
0
Emmy Sanga :
kwahiyo nayo yale manukato aliyopakwa Bwana yesu na yule aliyekuwa hahaha alikuwa anaeneza uzinzi kwa nani sasa,mmmhmmm hii Biblia tuombe hekima ya roho mtakatifu atufunze kwa sahihi tusikulupuke nayo ,yeeeeeeh
2026-07-28 08:14:52
3
My Name :
MUNGU akutienguvu zaidi hatawakipinga ukweli unabaki palepale
2026-07-08 14:21:17
1
Rehemat Tarimo's :
hatimae nimepata jibu la swali langu! Ahsante mtumishi wa Mungu kwa ujumbe wako kwangu.
2026-07-03 20:56:49
1
queensly7 :
imeandikwa wapi Kwa bibilia?
2026-08-24 11:34:46
0
Barakaboy :
mmmmmm mambo ni meng kwelikweli
2026-08-26 08:47:59
0
Salome Renatusi :
Amina ubarikiwe
2026-07-03 09:50:44
0
Success Eliya :
Mbona utateseka sana utafika mbinguni upo hoi
2026-08-29 19:40:40
0
mentor :
vp kuhus mpira
2026-08-10 10:28:31
0
evangelist phoustine khaindi :
injili imeshinda wengi n Neema ituokoe
2026-08-15 17:19:22
0
Diacre Emmanuel :
naku kubali mimi, yaani vumbuwa kweli
2026-08-13 21:04:58
0
jonas sayuni :
uzur hakuna pafyum ninayotumia hapo au sijaelewa swal
2026-08-27 15:34:23
0
Asimwe :
we kaka bado hajasema 😁😁😁😁
2026-08-30 04:12:36
0
Madame je ♥️💍 :
Uwe unaweka namaandiko yanayo kataza
2026-08-14 06:19:34
0
Tedy :
ndo maana najiuliza kwa Nini najichukia..
2026-08-22 13:33:40
0
dorkax :
kweli kabisa
2026-07-03 09:53:38
0
To see more videos from user @pastor_kagoro_01, please go to the Tikwm
homepage.