@eliyajames558: *MBINGUNI MAKAO YETU YA MILELE*Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.Dunia hii tunayoishi sasa imejaa maumivu, vilio, magonjwa, na utengano unaoletwa na kifo. Hata wakati tunapopata furaha, bado inakuwa ya muda mfupi kwa sababu mazingira ya ulimwengu huu yameharibiwa na dhambi. Sisi sote hapa duniani ni wasafiri na wapitaji tu; nchi hii si nyumbani kwetu.Lakini Biblia inatupatia tumaini kuu linaloweza kufuta kila chozi na kutia nguvu miguu yetu iliyochoka. Ahadi tuliyonayo ni kwam