@msemajiwamagari: SABABU 10 ZINAZOSABABISHA GARI KULA MAFUTA MENGI๐๐ 1. Air filter chafu โ Hupunguza hewa inayoingia kwenye engine, hivyo ECU huongeza mafuta ili kufidia upungufu wa hewa. 2. Spark plugs zilizochoka โ Mwako wa mafuta haukamiliki, hivyo mafuta mengi hupotea bila kuzalisha nguvu ipasavyo. 3. Oxygen (O2) sensor mbovu โ ECU hupokea taarifa zisizo sahihi na kuingiza mafuta mengi kuliko yanavyohitajika. 4. Matairi yenye presha ndogo โ Huongeza rolling resistance, hivyo engine hulazimika kutumia nguvu na mafuta zaidi. 5. MAF sensor chafu au mbovu โ Hupima vibaya kiwango cha hewa kinachoingia kwenye engine na kusababisha matumizi makubwa ya mafuta. 6. Thermostat mbovu โ Engine hushindwa kufikia joto sahihi la kazi, hivyo ECU huendelea kuongeza mafuta kama vile engine bado ni baridi. 7. Fuel injectors chafu au zinazovuja โ Hunyunyiza mafuta kwa kiwango kisicho sahihi na kuongeza matumizi. 8. Mtindo mbaya wa kuendesha โ Kasi kubwa, kuongeza mwendo kwa ghafla na kubana breki mara kwa mara huongeza matumizi ya mafuta. 9. Huduma za gari kuchelewa โ Kutobadilisha engine oil, filters na kufanya service kwa wakati hupunguza ufanisi wa engine. 10. Mzigo mkubwa usio wa lazima โ Kadri uzito wa gari unavyoongezeka, ndivyo engine inavyotumia mafuta mengi zaidi. Kumbuka: Gari likianza kula mafuta kuliko kawaida, usikimbilie kuuuza gari. Mara nyingi tatizo huwa kwenye matengenezo kidogo tu.๐๐๐ ๐ Kama unapenda kupata elimu na kujua gari gani zuri utaanzia maisha karibu kwenye group letu utachangia 5000 tu ya WI-FI ili nisipotee online๐ค๐ Chukua namba kwenye profile au nitumue sms dm nikuunge boss wangu๐๐๐โ
๏ธโ
๏ธ #WATUWEMABADOWAPO #SINATAMAANAPESAZAWATU #msemajiwamagari
Msemaji wa magari
Region: TZ
Saturday 04 July 2026 11:56:38 GMT
Music
Download
Comments
Nyokalongo :
sababu zote nazikubali ila sio no 6
2026-07-06 18:00:57
1
Ramadhan Juma :
safi
2026-07-05 06:13:37
1
Samy cosmetics :
Allex gari naipenda sana
2026-07-04 19:29:55
1
Chuse 360 :
sisi wa 27 to 30 km per liter tunacoment wapi
2026-07-05 06:53:59
1
shbn nyoni :
tairi low pressure ilikua 7.9perkilometre
2026-07-04 13:10:02
1
jimmy king :
jinq lq wimbo tafathal
2026-07-04 13:00:20
1
Sylivester Nyagwisi :
0629669798 niunge boss
2026-07-07 03:26:26
1
Mr.money :
Runx ,alex ni gar unyama saana mim naipenda kila nikitaka kuiuza nagaili
2026-07-07 08:59:48
1
To see more videos from user @msemajiwamagari, please go to the Tikwm
homepage.