@dunialeo_: Aliyekuwa kada wa CHADEMA, Charles Odero, amemtaka Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, kuepuka ushawishi wa makundi mbalimbali ambayo, kwa madai yake, hayana lengo la kufanikisha maridhiano ya kisiasa nchini. Akizungumza na waandishi wa habari, Odero alidai kuwa baadhi ya wanaharakati, wafanyabiashara wakubwa wa mafuta pamoja na makada wa CCM wanajaribu kumshawishi Heche kupinga ajenda ya mazungumzo na maridhiano ya kitaifa.#dunialeoUPDATES