@dunialeo_: Akizungumza na Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam leo, Jumapili tarehe 05/07/2026, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mussa Mohammed Makame amesema Tanzania haijashuhudia changamoto ya upatikanaji wa mafuta katika kipindi chote tangu kuanza kwa vita Mashariki ya kati, na hiyo inakuja hata kwa kufanya ulinganifu baina ya Tanzania na mataifa jirani, hatua ambayo imetimiza lengo la kwanza la serikali la kuhakikisha Nchi haipati uhaba wa bidhaa hiyo. Pia ameongeza kwa kusema kuwa Ugomvi wa kibiashara baina ya makampuni ya uagizaji wa mafuta unasababisha kuenea kwa taarifa nyingi za upotoshaji lakini Serikali inafanya jitihada kubwa za kuhakikisha mafuta yanapatikana nchini kwa wakati wote.#dunialeoUPDATES